Kagera: Muuguzi mbaroni kwa tuhuma za kuua mwanafunzi wakati akimtoa mimba

Kagera: Muuguzi mbaroni kwa tuhuma za kuua mwanafunzi wakati akimtoa mimba

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Jeshi la Polisi mkoani Kagera, linamshikilia Dezber Kahwa (49), mkazi wa Kijiji cha Kibengwe, Bukoba Vijijini, kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Alinda Leverian (14), mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Kilima, kwa kumtoa mimba kienyeji.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi, alidai jana kuwa tukio hilo lilitokea Februari 8 mwaka huu nyumbani kwa Vedastina Cleophace baada ya Kahwa kujaribu kumtoa mimba mwanafunzi huyo.

Alidai kuwa Kahwa aliwahi kuwa muuguzi katika Zahanati ya Buzi, lakini alifukuzwa kazi na serikali wakati wa uhakikiwa wa watumishi hewa na wenye vyeti feki kutokana na kutokuwa na cheti cha kidato cha nne.

"Mtuhumiwa huyo alikuwa hana cheti cha kidato cha nne, ulipofanyika uhakiki wa watumishi hewa, akafukuzwa kazi na serikali lakini akaendelea kuhudumia wagonjwa mtaani bila kibali na kwa kificho, na wakati mwingine alifanyia shughuli hizo nyumbani kwake," alidai.

Kamanda Malimi alidai kuwa baada ya jaribio hilo, binti huyo alipata maumivu ya tumbo na kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa, ambako inadaiwa alipatiwa matibabu ya maumivu ya tumbo, kitendo ambacho ndugu na jamaa wanahisi ndiyo sababu ya kifo chake.

"Mtuhumiwa amekamatwa na anaendelea kuhojiwa na polisi, lakini tayari mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari wa binadamu katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Kagera na uchunguzi wa awali umebaini chanzo ni kutobolewa kwa mfuko wa uzazi na kuingizwa dawa sumu," alidai.

Katika tukio lingine lililotokea Februari 9 mwaka huu majira ya saa tano usiku katika Mtaa wa Rwazi, Kata ya Kahororo, Manispaa ya Bukoba, mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kahororo, Buberwa Mberwa (14), alifariki dunia baada ya kudaiwa kujinyonga kwa kutumia mkanda aliokuwa akiutumia kufungia suruali.

"Alikutwa amejitundika kwa mkanda ambao alikuwa akiutumia kufungia suruali, aliufunga katika nondo ya dirisha, katika nyumba hiyo alikuwa akiishi na mama yake pekee, baada ya baba yake kuwatelekeza na kusababisha hali yao ya maisha kuwa ngumu," Kamanda Malimi alidai.

Kiongozi huyo wa Jeshi la Polisi alidai taarifa kutoka eneo la tukio zilidai kuwa, kabla ya tukio hilo, majira ya saa 12 jioni, mwanafunzi huyo aliporejea nyumbani, aliwakuta watoto wa baba yake mdogo ambao ni pacha; Kakuru Laurent (8) na Kato Laurent (8), wanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Kahororo, wakichezea mkanda huo, na kuwa aliwataka wampe mkanda wake wakamkatalia.

"Lakini walipomwona kachukia, waliamua kumpa mkanda wake na kuondoka kwenda kwao na baadaye ndipo ikabainika kuwa amejinyonga," alidai.

Kwa mujibu wa Kamanda Malimi, mwanafunzi huyo aliwahi kuwa na tatizo la afya ya akili.

Chanzo: IPP Media
 
na hao wazazi wa huyo mwanafunzi wapatiwe hukumu
 
Back
Top Bottom