Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
Washitakiwa tisa (9) wanaotuhumiwa kuhusuka na mauaji ya kikatili ya mtoto mwenye ualbino Marehemu Noela Asimwe Novat aliyekuwa na umri wa miaka miwili na nusu mkazi wa kata ya kamachumu ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera wamefikishwa mbele ya jaji wa mahakamani kuu ya Tanzania kwa ajili ya kusomewa shitaka linalowakabili na maelezo ya awali ya kesi hiyo kabla haijaanza kusikilizwa.
Washtakiwa hao wamefikishwa mbele ya jaji wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Bukoba Emanuel Ngingwana aliyekubaliana na maombi yaliyowasilishwa na upande wa jopo la mawakili wa utetezi ya mtuhumiwa namba moja padri Elipidius Rwegoshora kutosomewa mashitaka yanayomkabili hadi atakapofanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa akili.
Jopo la mawakili wanne wa upande wa utetezi likiongozwa wakili msomi Projestus Mulokozi awali liliiiomba mahakama isitishe zoezi hilo kwa kuwa mteja wao kwa sasa hana uwezo wa kuongea vizuri pamoja na kuelewa anachokifanya kwa maana hiyo hawezi kujitetea kwa usahihi hivyo wakaomba kupokelewa kwa maombi ya upande wa utetezi
Aidha mawakili wa Jamhuri wakiongozwa na wakili wa Serikali mwandamizi, Waziri Magumbo anayeshirikiana na mawakili wengine wa Serikali ambao ni pamoja na Erick Mabagala na Matilda Assey hawakuweka pingamizi la aina yoyote walikubaliana na uamzi uliotolewa na mahakama wa kusikitisha zoezi.
Jaji Ngigwana aliamua mtuhumiwa apelekwe Isanga akapimwe akili hivyo,alieeleza kuwa watuhumiwa wote watasomewa mashtaka ya kesi inayowakabili kwa pamoja baada ya kupatikana matokeo ya uchunguzi wa ugonjwa wa akili wa mtuhumiwa namba moja padre Elipidius Rwegoshora ambapo kesi hiyo itatajwa tena Desema 11, 2024.
Watuhumiwa wengine ni Novat Venant (24) ambaye ni Baba mzazi wa mtoto Asimwe,Ramadhan Selestine, Nurdin Masoud, Rwenyangira Burukad, Dastan Burchard, Faswiu Athman, Gozibat Arikad na Dezdery Everigist amabo wote wamerudishwa Lumande.
Pia soma: Kifo cha Asimwe Novath (Albino); Baba mzazi na Paroko msaidizi washikiliwa kwa tuhuma za mauaji