Jeshi la polisi mkoani Kagera kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, mwaka huu limepokea magari mapya matano ili kuongeza nguvu na kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa Amani katika maeneo yote.
Akiongea na waandishi wa habari mjini Bukoba, kamanda wa polisi mkoa wa Kagera kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Blasius Chatanda amesema kuwa jeshi hilo litahakikisha uchaguzi huu unafanyika kwa usalama na Amani.
Ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua na kuzifanyia kazi changamoto za vitendea kazi ambavyo jeshi hilo lilikuwa likisumbuka.
Aidha Chatanda amewaomba wananchi wa mkoa huo kujitokeza kupiga kura ili kutendea haki haki yao ya msingi huku akiwahakikishia usalama wakati wote na baada ya uchaguzi.