Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Hizi ni rushwa kuwashawishi wananchi wafanye wafanye maamuzi, iwe kwa pesa au visheti vyote ni rushwa. Kwanini vinaachwa kuendelea kufanyika? TAKUKURU mnafanya nini?
===
Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amezunguka kwenye baadhi ya vijiwe vya Kahawa katika manispaa ya Bukoba akiwasihi wananchi kushiriki uchaguzi huo.
RC Mwassa katika mizunguko hiyo amebeba visheti alivyovitengeneza mwenyewe na kuwagawia watu kwenye vijiwe vya kahawa ikiwa ni ishara ya upendo huku akifikisha ujumbea wa kushiriki uchaguzi.
Kupata vimbwanga vingine wakati wa Uchaguzi ingia hapa: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Ametumia mwanya huo kuwashukuru wananchi wa Kagera kwa kujitokeza kushiriki zoezi la kujiandikisha na kuwaomba wale wenye sifa kuendelea kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali kwakuwa tayari pazia la kuchukua fomu limeshafunguliwa.
Ameongeza kuwa uchaguzi wa mwaka huu atahakikisha unakuwa wa huru na haki huku akiendelea kutoa onyo kali kwa wale wenye nia ya kuleta vurugu kuwa amejipanga kuwakabili.