Kagera: RC Mwassa awaita wananchi kwenye uzinduzi wa kampeni ya kitaifa kupinga ukatili dhidi ya maalbino. Waziri Ndejembi kuongoza uzinduzi huo

Kagera: RC Mwassa awaita wananchi kwenye uzinduzi wa kampeni ya kitaifa kupinga ukatili dhidi ya maalbino. Waziri Ndejembi kuongoza uzinduzi huo

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
RC MWASSA AWAITA WANANCHI KWENYE UZINDUZI WA KAMPENI YA KITAIFA KUPINGA UKATILI DHIDI YA MAALBINO. WAZIRI NDEJEMBI KUONGOZA UZINDUZI HUO.

Ni leo Jumanne Julai 09, 2024 kwenye Viwanja vya Kamachumu wilayani Muleba.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwassa leo anawakaribisha wananchi wote wa Kagera na Watanzania kwa ujumla kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kupinga ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino). Uzinduzi wa Kampeni hii utaongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Deo Ndejembi kwenye Uwanja wa Mpira Kamachumu karibu na kiwanda cha Maji Kabanga kuanzia saa 7 mchana.

Maalbino ni Binadamu kama Binadamu wengine na wana mchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya Taifa letu, wana haki ya kuishi kama wengine. Tuungane kupinga ukatili wa aina yoyote dhidi yao. Wote mnakaribishwa Muleba.

IMG-20240708-WA0006.jpg
IMG-20240708-WA0005.jpg
 
Back
Top Bottom