DOKEZO Kagera: Rushwa imetawala ofisi ya kata Nyaruzumbura, wilayani Kyerwa

DOKEZO Kagera: Rushwa imetawala ofisi ya kata Nyaruzumbura, wilayani Kyerwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Habari za Asubuhi ?

Ninatanguliza shukrani kwa jukwaa hili la fichua UOVU.

Nimewahi kwenda kupata msaada kwenye ofisi ya mtendaji wakata ya Nyaruzumbura , Wilaya Ya kyerwa, Mkoa Kagera, nilichokutana nacho huko kinatisha sana

Rushwa imetawala vyakutosha kuanzia kwa MTENDAJI WA KATA, MTENDAJI WA KIJIJI PIA MWENYEKITI WA KIJIJI, wakikaa kutengeneza suluhu wanatengeneza kwa kutafuta pesa zao mfukoni kana kwamba mtendaji wa Kata hawalipwi na serikali kwa ajili yakuhudumia wananchi

Kule katani wameamua kufanya sehemu ya kufungia watu na kuwapa adhabu za hapa na pale, kiukweli hilo jambo limeniumiza sana.

Ukienda pale lazima utoe kuanzia laki na kuendelea na wanakwambia baada ya suluhu na wao wanahitaji hela ya muda walioutumia pale kwenye suluhu jambo ambalo ukiwapa ile pesa haiandikiwi sehemu, binafsi niligoma kuwapatia kitu wakanitisha watanionesha

Hivyo Niombe Mkuu Wa Wilaya Kyerwa atembelee kuona yanayoendelea kwenye kata ya Nyaruzumbura maana Rushwa imekithiri kuliko sehemu zote nilizopita.

Afisa mtendaji wa kata anatumia madaraka kupiga watu na wakuonea na hana uwezo wa kusuluhisha maana ni mtu anayeegemea pande moja.

Yangu ni hayo.
 
Rushwa ni adui wa haki na maendeleo ya jamii. Kinachoendelea katika kata ya Nyaruzumbura ni ishara ya jinsi ufisadi unavyowakandamiza wananchi wasiokuwa na sauti.

Watendaji wa umma wanapaswa kuwa watumishi wa wananchi, si wakandamizaji wanaotafuta maslahi binafsi kwa kutumia nyadhifa zao. Kitendo cha kulazimisha watu kutoa fedha kwa ajili ya suluhu ni kinyume cha maadili na sheria.

Ni muhimu kwa mamlaka husika, hasa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika ili kurejesha haki na uwajibikaji katika utumishi wa umma.

Wananchi pia wanapaswa kuungana na kupinga vitendo hivi kwa kuripoti kwa vyombo vya juu vya sheria ili kukomesha uovu huu.
 
Back
Top Bottom