The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Jumla ya madawati 90 na viti vimetolewa kwa shule za sekondari na Wakala wa Uhifadhi Misitu Tanzania TFS wilayani Misenyi mkoani Kagera ili kuweza kuboresha upatikanaji wa Elimu kwa wanafunzi.
Akikabidhi madawati hayo Kamishina Kamanda wa TFS Kanda ya Ziwa Ebrantino Mgiye amesema kufanya hivyo ni sehemu ya utaratibu wa TFS kuchangia maendeleo katika taasisi za kiserikali.
Akipokea madawati hayo mkuu wa wilaya ya Misenyi mkoani Kagera Kanali mstaafu Hamis Maiga ametoa wito kwa walimu kuweka utaratibu wa kutunza madawati hayo.
Aidha madawati hayo yamegharimu zaidi ya mil 5.9 na kukabidhiwa kwa wakuu wa shule za sekondari ya Mutukula pamoja na Bunazi sekondari wilayani Misenyi mkoani Kagera.