Jovinus Mujuni
New Member
- Dec 18, 2024
- 2
- 2
Jamani hivi suala la kujengea wanafunzi vyoo ni jukumu la nani? maana Kuna shule moja wilaya ya Missenyi mkoani Kagerainaitwa Mugana A kwakweli hali ya vyoo sio salama kwa watoto wale kwani vimechakaa mno na havikidhi mahitaji yao kwani wataambulia kupata magonjwa.
Hivyo wahusika tunaomba hili suala muweze kulitilia maanani maana hizo ni afya za watoto wetu, kwanza vyoo havina miundombinu ya maji na suala hili limekuwa kero ya muda mrefu.
Hivyo kupitia jukwaa hili naomba wahusika muweze kulivaa hili na kuweza kuwasaidia watoto hawa kupata vyoo safi na vya kisasa.