DOKEZO Kahama Mgomo wa wafanyakazi wa barabara wasababisha ukosefu wa maji kwa wiki mbili sasa

DOKEZO Kahama Mgomo wa wafanyakazi wa barabara wasababisha ukosefu wa maji kwa wiki mbili sasa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mbishi Uswazi

Senior Member
Joined
Feb 7, 2020
Posts
170
Reaction score
315
Wakazi wa Wilaya ya Kahama kata ya Majengo, ni wiki ya pili sasa kaya zaidi ya 400 hazina huduma ya maji kutokana na mgomo wa wafanyakazi, wakidai malimbikizo ya mishahara kwa mkandarasi, walikata bomba kubwa linalosambaza maji kwa ajili ya kulihamisha.

Baada ya kulihamisha hawakuunganisha mabomba ya watu waliyoyakata na vifaa vya kuunganishia mabomba waliondoka navyo ndo wakaanza mgomo.

Ni wiki ya pili leo tunaomba mamlaka husika zitusaidie watuunganishie maji maana hatujui mgomo wao unaisha lini tunaangaika na maji.
 
kahama miundo mbinu ni shida, hasa barabara
angalia barabara inayotoka phantom kuingia mjini , inazibwa viraka kwa udongo
barabara inayoingia anderleck shuleni utafikiri serikali haipo ni mbovu ina michanga balaa
 
Ni ajabu sana mzee kila mwezi wanaziba viraka kwa udongo wa simenti na mchanga
 
Back
Top Bottom