Kwahiyo lile gari alilotoa Rais Samia kupitia Makonda kwa yule shehe Arusha, TAKUKURU.... au basi!
====
Your browser is not able to display this video.
Kuelekea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 Mwaka huu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Kahama imesema itachukua hatua za kisheria kwa wagombea watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa sambamba na matumizi ya wapambe (machawa) wanaotumika kugawa fedha na zawadi ili kuhamashisha wagombea wao waweze kuchaguliwa.
Kauli hiyo imetolewa Afisa Sheria wa TAKUKURU, Mlamuzi Kuhanda wakati na wadau wa sekta ya habari katika kikao kilichokuwa na lengo ya kuwaomba kushirikiana nao katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa huku mkuu wa taasisi Wilaya ya Kahama, Abdallah Urari akisisitiza juu ya uzingatiwaji wa sheria.