Kahama VS Njombe/Mafinga

Wacha kazi ziendelee
W
 
Takataka tuu unaongea.

Hivi unajua Serikali inajenga viwanja vya ndege vingapi Iringa na Mbeya?
 
 
TAWI LA CHUO KIKUU DODOMA KUJENGWA NJOMBE

Tarehe Iliyowekwa: December 22nd, 2023
Kikao cha Kamati ya Ushauri na Maendeleo (RCC) Mkoani Njombe kilichoongozwa na Mkuu wa Mkao wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka Disemba 22,2023, kimeridhia kujengwa Tawi la chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) katika makao makuu ya Mkoa Mjini Njombe.

Akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe Profesa Lughano Kusiluka Makamu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) amesema katika utafiti wa maeneo ambayo yaliyoorodheshwa wamebaini kuwa maeneo ambayo yatafaa kwa ajili ya ujenzi wa chuo kikuu ni eneo la Shule ya Sekondari Njombe (NJOSS) na Ihalula yaliyopo Halmashauri ya Mji Njombe ,kutokana na maeneo hayo kukidhi vigezo kulingana miongozo ambayo inatakiwa kutumika.

Akiendelea kuzungumza Profesa Lughano amesema chuo kikuu cha Dodoma kitakachojengwa Njombe kitachukua kozi za ufugaji ,kilimo,Mawasiliano na teknolojia.

Anthony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa Njombe amemshukuru Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha ambazo zita jenga chuo kikuu Mkoani Njombe huku akiwaomba wadau ambao wamehudhuria kikao hicho kutumai fursa mbalimbali za uchumi katika uwekezaji ambao utaleta ushindani wa uchumi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Mhe.Deo Mwanyika na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe Erasto Mpete kwa pamoja wamesema, wameridhiswa na maeneo ambayo yametengwa na kuchanguliwea kwa ajili ya ujenzi wa chuo kikuu jambo ambalo litaleta chachu ya maeneleo katika Mkoa wa Njombe.
 
Wakati Kahama na Bukoba wanalingishia Vi Airstrip wakae wakijua kwamba Kubwa lao linakuja Njombe.

Uwanja utakuwa na
-3km runway
-Passenger Building
-Cold facilities


UWANJA MKUBWA WA NDEGE KUJENGWA NJOMBE

Tarehe Iliyowekwa: October 28th, 2023
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philip Isdor Mpango, amesema serikali imepanga kujenga uwanja mkubwa wa ndege Mkoani Njombe.

Mheshimiwa Mpango ametoa kauli hiyo ya serikali Oktoba 28,2023 wakati akihitimisha maonesho ya nne ya Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO yanayofanyika kitaifa mkoani Njombe.

Amesema serikali inatambua fursa mbalimbali zilizopo mkoani Njombe na umuhimu wa usafiri na usafirishaji hivyo serikali imeamua kujenga uwanja mkubwa wa kisasa wa ndege Mkoani Njombe.

Mheshimiwa makamu wa Rais amesema kuwa ujenzi wa uwanja wa ndege Njombe utahusisha ujenzi njia ya kurukia ndege yenye urefu wa kilometa Tatu (3), Jengo kubwa la abiria na Jengo maalumu kwa ajili yakuhifadhi bidhaa zinazoharibika haraka.

"Sisi serikali tunaamini uwepo wa usafiri wa uhakika utachangia kuinua na kukuza uzalishaji viwandani na mashambani lakini pia kuinua sekta ya utalii mkoani Njombe."Alisema Mheshimiwa Mpango.

Uwanja wa ndege utakao jengwa mkoani Njombe utakuwa na uwezo wa kupokea ndege kubwa za abiria pamoja na ndege za mizigo.
 
#TAARIFAYAMKURUGENZI

NDC kwa mwaka wa fedha 2023/2024, limepanga kutimiza maono ya kutekeleza Mradi wa Liganga na Mchuchuma ambao kwa miaka mingi ulikuwa ikikabiliwa na mikwamo licha ya kuwa na manufaa makubwa kwa uchumi wa nchi kwa kufanya mambo yafuatayo:

i. Kukamilisha majadiliano na mwekezaji na kusaini Mkataba wa Ubia. Majadiliano hayo yanategemea kukamilishwa ndani ya mwaka wa fedha 2023/2024 na hivyo kuruhusu hatua zinazofuata za uwekezaji,

ii. Kuanza uchimbaji wa Makaa ya Mawe kupitia makampuni matano (5) ambayo yamepatikana mwaka wa fedha 2022/2023. Jumla ya tani 315,000 za Makaa ya Mawe zinatarajiwa kuchimbwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 kwa Mradi wa Mchuchuma,

iii. Kulipia Ada ya Mwaka (Annual rent) kwa Leseni Ndogo za Uchimbaji nje ya leseni kubwa katika Mradi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma. Baada ya malipo hayo, Kampuni zinaruhusiwa kuendelea na uchimbaji wa Makaa ya Mawe.

#ndc #SHIRIKALATAIFALAMAENDELEO #NATIONALDEVELOPMENTCORPORATION
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…