Kahama VS Njombe/Mafinga

Karibuni kwenye mada.

Nawiwa kuilinganisha na kushindanisha mji wa Kahama na Njombe au Mafinga.

Je, ni mji gani mzuri na una future kubwa kifursa kuliko mwenzie in terms of maendeleo na ukuaji?
Tuwekee picha bwana pamoja na wasifu wa hizo sehemu....we vipi? Sasa hapa tutajadili nini, kuna wengine hatujafika hizo sehemu.
 
Mtu kwao ndio imetawala katika malumbano yote haya,Njombe iko mbali sana kwa Kahama na Mkuu amesema wazi ametoa zawadi ya manispaa kwa sababu alipewa kura nyingi hapo Kahama,lakini kuna mazoea ya watu humu kusifia sana kwao na kudharau sana maeneo mengine,maeneo mengi yanafanana tu,baadhi ya maeneo yalipata upendeleo kwa sababu ya watu fulani waliokuwa na nguvu katika nafasi zao lakini vijana wanakuja na nyodo nyingi na kupinga maendeleo ya sehemu nyingine mpaka inashangaza kama wote hawa ni watanzania kweli? du JF inaonyesha picha halisi mioyo ya watu.
 
Tajiri Giningi wa kwanza.. 🙂
Punguza stress Mkuu... Have fun
 
Unasema ulikuwa Kahama januari hii,ukaielewa Kahama na ndipo unaitetea sana lakini hujasema umewahi kufika Njombe,kwa hiyo cha maana katika arguments zako.Wewe ni sawa na vipofu waliomgusa tembo,aliyegusa sikio alisema tembo mkubwa kama beseni,aliyegusa mkia alisema tembo mkubwa kama fimbo,Wewe umetoka Tanga ukaona Kahama basi mji mkubwa kuliko mji wowote,du wabongo pata exposure kidogo.
 
inachekesha wanaongea tu,hata aliyeleta mada naye hana picha hata moja.
Acha uvivu unadakia kwa mbele afu unadai picha? Anza kuperuzi ukurasa Hadi ukurasa utazikuta picha kibao sema picha za current ndio bado hatujaweka
 
Kahama imepewa hadhi ya manispaa kisiasa.

Njombe na Mufindi ni wilaya mbazo zipo kwenye top.10 tajiri kitaifa.

Kahama kuna maskini wengi sana ndio maana mbunge wao hadi ameomba wizara iruhusu wanafunzi kwenda na viporo shuleni, jambo ambalo huwezi lisikia kwenye mji kama Njombe, makambako, mafinga etc.
 
Kahama
Dodoma

 
We hauna argument unatereza tu..

Unavijua vigezo vyakuwa manispaa!?

Utajiri wa wilaya sio utajiri wa mji.. soma hiyo kwanza.. mjini hakuna mashamba mjini watu wanaenda kazini sio shambani..

Sasa ukiangalia kwa kigezo hicho hapo NJOMBE wangapi wanaenda kazini!?
 
Khm ilikuwa kibiashara za magendo container za nje kushushwa zama zile na kufanya kituo cha kanda kununua mizigo ya jumla.
Miundombinu mibovu awali Mikoa Tabora,Katavi,Kigoma, sasa mikoa hiyo inamiundombinu mbadala kuunga na Bandari.
Ujio wa std gauge utapunguza kabisa malori intransit tegemeo la Khm.
Khm inasehemu ndogo s ana madini, zaidi halimashauri ya Msalala ambapo mgodi wa Bulyanhulu, Isaka vipo, ambayo ikipata wapiga debe itapata wilaya mpya.
Khm ni pakame pana awali panategemea Tabora,halmashauri ushetu na Msalala, Wilaya mpya Mbogwe ilimega eneo bora la kilimo pia.
Wengi waliwekeza khm kwa sababu miundombinu,huduma, usalama, tuendako miji midogo inaimarika.
 

Jiji inatakiwa square kms 250 upwards idadi kweli Kahama wamekidhi kigezo cha idadi , swali linakuwa je Kahama wana eneo hilo la mji ?
 
Kunywa pepsi ntalipa,umemaliza yote
 
Kahama ingekuwa mjini si tungeona magorofa kushinda Njombe? Kahama ni kijiji kikubwa cha wachuuzi
 
Jiji inatakiwa square kms 250 upwards idadi kweli Kahama wamekidhi kigezo cha idadi , swali linakuwa je Kahama wana eneo hilo la mji ?
Vigezo vya kuupa mji hadhi ya Manispaa au jiji kwa bongo ni hovyo kabisa imagine mji wa hovyo hovyo kama kahama eti nao ni manispaa ,hivi ni vichekesho
 
You have spoken it right ,agiza gambe nalipa sasa hivi.Huo mji umeshadumaa sasa hakuna jipya zaidi ya kuzaana kuongeza maskini tuu hapo
 
Just imagine watu wanashindia viporo yaani ni aibu eti Magu ndio anaita Mnispaa kisa home si bora hata Kasulu ingekuwa Manispaa
 
Kahama ni Soko.. na strategically hakuna mji uko katikati ya the greater east Afrika zaidi ya Kahama let that sink..

Ujenzi wa the biggest smelting plant kwa Afrika ya Mashariki na kati umezingatia hilo... Ndio maana bila kushurutishwa Wabia wa miradi wamechagua Kahama..

Muwekezaji wa Kahama kwenye uzalishaji ana advantage kubwa yakifikia soko kubwa zaidi (Market catchment) umbali wa kilomita 600 both directions kutokea Kahama unakuwa kwenye miji mikubwa mingi ikiwemo Kisumu, Kigoma, mwanza, bukoba, kigali, Bujumbura, Kampala, Dodoma, tabora nk.

Kuna mtu anauliza 70m USD manufacturing establishment unaenda kufanya nn, kwa kifupi soko liko.. kubwa.. kama jambo kapenetrate kiasi cha kuififisha Azam na Kilimanjaro kanda ya ziwa unadhani nn kinashindikana!?

Kwa kifupi hata watu kuamua kwenda kufanyia hayo magendo Kahama ilikuwa ni kwa sababu.. kwamba isiwe Nzega au tinde !? Kwa ss Kahama imekuwa destination Town.. ni yenyewe ndio inayogenerate trips sio kutegemea wanaopita.

Wafanyabishara wengi wa burundi na Rwanda tayari wamekwisha anza kushuka Kahama na kugeuza kwa mahitaji mengi.. na mawakala wakubwa wa wazalishaji wakubwa nchini wamekwisha anza kuchukua position...

Najua mpaka muone barabara za mataa na magorofa ndio mnaona mji wa maana... Juzi tu Arusha Mianzini na Iringa miyomboni yalikuwa mahandaki.. it takes one move and all that is gone... and that move ndiyo iliyofanyika jana... Hushtuki ugeni mkubwa kiasi kile kwa mji wa hovyo!?

Kahama imekwisha vuka threshold hakuna namna it will ever be doomed... Ndio lishawaka hilo inakwenda na itafika... Same case ya Moshi na Arusha...inajirudia.. de javu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…