MICHUZI BLOG AT
WEDNESDAY, JULY 03, 2024 MAKALA,
Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Makambaku
UKWELI ni kwamba Bohari ya Dawa (MSD) imedhamiria kuhakikisha inaendeleza mkakati wake wa kuzalisha bidhaa za afya ikiwemo mipira ya mikononi maarufu โglavesโ.
Ukiwa katika kiwanda chake cha kuzalisha glaves kilicopo eneo la Idofi Halmashauri ya Makambako mkoani Njombe utashuhudia kiwanda hicho ambacho ujenzi wake ulianza Oktoba 4, 2020 kikiendelea na uzalishaji ulioanza rasmi Februari mwaka huu na hadi sasa jozi milioni mbili za glaves zimeshatengenezwa.
Ni wazi MSD chini ya uongozi mahiri wa Mkurugenzi Mkuu wake Mavere Tukai imeamua kubeba kwa vitendo dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kiwanda cha Gloves Idofi kinazalisha mipira ya mkono na hatimaye kuokoa fedha ya serikali iliyokuwa ikitengwa kuagiza mipira hiyo nje ya nchi.
Akizungumza na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliotembelea kiwanda hicho, Mhandisi Shiwa Mushi ambaye ni Kaimu Meneja Kiwanda cha Glovu MSD Idofi anaeleza hatua kwa hatua kuhusu sababu za kuanzishwa kwa kiwanda hicho na uzalishaji unaoendelea kwa sasa.
HISTORIA YA KIWANDA
Kwa mujibu wa Mhandisi Mushi, kiwanda hicho kinamilikiwa na MSD na kilianza kujengwa Oktoba 4, mwaka 2020 na dhumuni la kujengwa kwake ni kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Uviko-19 mwaka 2019.
โWakati wa janga la Korona miongoni mwa changaoto tulizozipata kama taasisi na nchi kwa ujumla ni uingizaji wa vifaa tiba nchini, kutokana na vizuizi na uagizaji wa dawa ilikuwa changamoto kubwa.
โKwa hiyo nchi ikaona kuna haja pia kuanza kuanzisha viwanda vyake hasa kutokana na somo ambalo tumelipata na tukaona kiwanda cha aina ya glaves ni muhimu tukaanza nacho kwasababu tumekwenda kwenye changamoto ya upungufu wa vifaa tiba nchini.
โNa ukiweza kuvaa glaves utaweza kuwahudumia wagonjwa hata kama ni wa Korona kwa usalama zaidi. Kwa hiyo tukaanza na kiwanda cha gloves ambacho kimejengwa Idofi, Makambako katika eneo lenye ukubwa wa ekari 38 na MSD inalimiki kisheria na ililitwaa kutoka kwa wananchi wa Idofi, tumewalipa na sasa eneo hili lina hati.โ
MAJENGO YALIYOPO
Mhandisi Mushi anaeleza katika eneo hilo la kiwanda kuna majengo mengi yanayotoa picha ya kiwanda hicho na jengo hilo la kiwanda lina urefu wa mita 130 na upana mita 124 kwa maana kwamba ukiangalia mita za mraba 3,120.
Anasema katika hayo majengo lipo jengo la malighafi kwa ajili ya uzalishaji na majengo mawili mengine wamepanga yatakuwa kituo cha kiwanda cha gloves na wakiendelea na uzalishaji vizuri na kufanya biashara watajenga majengo mengine.
โKwa upande wa kulia kwenye michoro yetu kuna majengo ambayo kwa sasa yapo kwa ajili ya uhifadhi wa bidhaa,โ anafafanua.
AINA MBILI ZA GLOVES
Pamoja na hayo anasema mikakati ya kiwanda ni kuzalisha aina mbili za glaves ambazo ni Surgical glove (zinatomika kuvaa kwenye upasuaji) na Examination glave (Glavu zinazovaliwa wakati wa uchunguzi wa awali).
KIMEBAKISHA SEHEMU MBILI
Akitoa maelezo zaidi ya kiwanda hicho, Mhandisi Mushi anasema kimebakisha sehemu mbili katika mkakati wa uzalishaji huku akifafanua kuwa kinakwenda kuzalisha pisi 20,000 ambazo ni sawa na pea 10,000 na hiyo ni kama kinazalisha katika hali yake ya kawaida.
โNa kiwanda hiki ukifanya mahesabu kitaalamu inaonesha kwa mwaka kitazalisha jumla ya glaves jozi milioni 86.4, ambazo ni sawa na asilimia 86.34 ya mahitaji ya nchi.
โKwa hali hii unaweza kuona kiwanda hiki ni kikubwa kwa kiasi gani, na sasa tumebaki na uzalishaji wa Examinationa glaves, ambapo katika kuzalisha kunahitajika malighafi.โ