Tunatakiwa kujenga taifa la watu wastaarabu, wanaoheshimiana, watu wa haki, wenye busara na wamoja kwa mustakabali mwema wa taifa.
Haya mambo ya kukosa mifumo mizuri ya haki na uwazi katika uchaguzi yanaharibu jamii, yanajenga unyama na mgawanyiko usio wa lazima.
Ni lazima kujenga undugu, umoja, na mshikamano. Vyama ni majukwaa ya kufanyia siasa za maendeleo ya wote kwa faida ya taifa zima.
Adui mkubwa wa taifa siyo vyama vyama siasa, ni watumishi wa Uma na vyombo vya dola wasiotumia akili na kutenda haki.