Kahawa ni moja ya nyara za Serikali

Kahawa ni moja ya nyara za Serikali

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Nani mmiliki wa kahawa Tanganyika? Serikali au mkulima?

Kwa nini Serikali inatumia nguvu nyingi sana kuzuia wakulima kwenda kuuza kahawa yao Uganda, mahali wanakoamini kuwa watapata faida nzuri?

Serikali ya Tanganyika inaionea Uganda wivu?

Serikali haitaki raia wake "watajirike"?

Ni mbinu za wahasimu wa mkoa wa Kagera wenye nia ya kuukandamiza mkoa wa Kagera kiuchumi ili waendelee kuusimanga kuwa ni mkoa maskini ilhali ni "nchi" iliyobarikiwa?

Nani mnufaika wa hizo harakati za Serikali kuwazuia wakulima wa kahawa kwenda kuuza mazao yao kwenye soko zuri na la uhakika?

 
kuna mtu alinifundisha kuwa kadri unavyozidi kuwa mkubwa uwezo wako wa kutumia akili unapungua na unabaki kutumia busara na hekima.

uchumi unajengwa kwaakili na maarifa pia tekinolojia.

Sasa sisi tunaendelea kuwaruhusu na kuwakubali watu walewale toka wakiwa vijana na sasa wanavitukuu kuwachagua kama viongozi wetu halafu tutegemee twende na kazi ya mabadiliko! hata kidogo;

wacha tuumizwe labda mbele tutapata akili ya jinsi ya kubeba mzigo tuliotwishwa na watwana wetu. kwakuwa siku zote tumekubali tufanye mambo yote kwa hekima na busara.

tukumbuke busara hupanda ngazi na huogopa tekinolojia ndio maana haipandi lift.
 
Kahawa ukiuza nje unahujumu uchumi ni zao la biashara
Kahawa inakausha
Kahawa inakobolewa
Kahawa inafanyiwa pa cm packaging
Kahawa inasafirishwa

Yote haya yakifanyika nchini yanatengeza chain ya pesa na ajira
 
Back
Top Bottom