kuna mtu alinifundisha kuwa kadri unavyozidi kuwa mkubwa uwezo wako wa kutumia akili unapungua na unabaki kutumia busara na hekima.
uchumi unajengwa kwaakili na maarifa pia tekinolojia.
Sasa sisi tunaendelea kuwaruhusu na kuwakubali watu walewale toka wakiwa vijana na sasa wanavitukuu kuwachagua kama viongozi wetu halafu tutegemee twende na kazi ya mabadiliko! hata kidogo;
wacha tuumizwe labda mbele tutapata akili ya jinsi ya kubeba mzigo tuliotwishwa na watwana wetu. kwakuwa siku zote tumekubali tufanye mambo yote kwa hekima na busara.
tukumbuke busara hupanda ngazi na huogopa tekinolojia ndio maana haipandi lift.