Kahawa ya kupunguza unene ya Brazil

Kahawa ya kupunguza unene ya Brazil

damian marijani

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2010
Posts
695
Reaction score
466
Kuna hii kahawa ya kupunguza unene (Slimming coffee) inayotoka Brazil. Inatumia jina la kibiashara la Green Coffee. Taarifa za kuaminika zinaonyesha kuwa kahawa hii ina dawa aina ya sibrutamine. Dawa hii iliondolewa sokoni na shirika la kudhibiti madawa na chakula la Marekani (FDA) oktoba 2010 kwa sababu za usalama wa kiafya kama ifuatavyo:
sibrutamine inasababisha msukumo wa damu mwilini (blood Pressure) kupanda, mapigo ya mishipa (pulse) kuwa juu na kuwaweka hatarini wagonjwa wa moyo kama wale wenye mioyo hafifu (heart failure) na wenye magonjwa ya mishipa ya damu kwenye moyo (coronary heart disease) na wale waliowahi kupata kiharusi (stroke).
Bidhaa hii inaweza kuathiri maisha ya watumiaji hasa ambao watakaoitumia bila kupata ushauri wa wataalamu wa tiba au lishe.
 
Mkuu.@damian marijani Hiyo Kahawa uliyotaja haifai hata hapa kuitangazia kwa sababu ina madhara kwa binadamu wewe umeleta hapa watu sasa wataanza kuitafuta wakati ina dhuru binadamu.

1295264577_73199791_1-Pictures-of--BESTSELLER-NEW-LEISURE-18-SLIMMING-COFFEE-VERY-EFFECTIVE.jpg





DSCN2184.JPG
 
Back
Top Bottom