Atlast nimempata
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 386
- 680
Ndugu wanajamii forum. Nina jamaa yangu mmoja ni mtumishi katika taasisi moja maalufu hapa nchini amefanyiwa vitendo vinavyoonyesha chuki dhidi yake ili labda kumlazimisha aandike barua ya kuacha kazi na kupoteza haki zake.
Sheria ya ajira na uhusiano kazini ya mwaka 2004; Kanuni za ajira na uhusiano kazini za mwaka 2007; Sheria ya usalama na afya mahala pa kazi ya mwaka 2003 na marekebisho yake; vyote vimetaja kuwa mfanyakazi anazo haki nyingi ambazo anapaswa kuzifahamu na kuzipata.
Huyu jamaa yangu karibu haki zake zote kanyanganywa na mwajili wake. Ilipelekea akatengenezewa na kuzushiwa kesi ikapelekwa mahakamani akashinda. Kuona hivyo jamaa kazini pakawa hapakaliki.
Kaandika barua ya malalamiko kwa mwajiri bila kupata msaada wowote zaidi ya kujibiwa na kutuhumiwa zaidi. Jamaa kuona hivyo kaomba wiki moja akaangalie familia kama njia ya angalau atulize akili.
Alivyoondoka akazidisha siku tano lakini katoa taarifa kwa mwajiri kuwa anaumwa na vielelezo vya hospitali anavyokanionyesha. Baada hizo siku 5 kaandikiwa barua ya kufukuzwa kazi.
Jamaa yangu huyo akafurahi bora wamepata sababu ya wao waterminate mkataba wamlipe haki zake atafute maisha sehemu nyingine.
Chakusikitisha hata kabla ya kumpa barua ya termination wakazuia mshahara wake na sasa mwezi wa pili hana mshahara wala barua ya termination.
Sasa wana jamvi, ni SHERIA IPI YA KUZUIA MSHAHARA WA MTUMISHI bila kumpa barua au kuterminate mkataba unaoonyesha haki zake?
Jamaa yangu tayari anajiandaa kwenda mahakamani lakini ana uzoefu wa huku nyuma wa karibu watumishi wengi wakishitaki hiyo taasisi ikishindwa ukimbilia kukata rufaa ili kuchelewesha haki zao.
Sasa kwa wenye uzoefu wa sheria za kazi mnamshaurije huyu jamaa yangu kushinikiza apewe termination letter kwasababu bila shaka itaambana na haki zake au kama hakuna aweze kuzidai mahakamani.
Sasa hivi hajalipwa mishahara mwezi wa pili na mwajili hataki kumpa termination letter.