Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Kaimu Mkenyenge ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa TASAC amesema Serikali imekuwa inawekeza fedha nyingi bandarini kila mwaka lakini faida inayopatikana ni ndogo.
Amebainisha kuwa uchumi wa sasa wa kidunia unapaswa kushirikisha sekta binafsi, na lazima watu wenye uzoefu watafutwe ili wasaidie wakati Serikali ikiendelea kufuatilia kwa ukaribu shughuli hizo za uendeshaji bila kulala.
Bandari ni lango kuu la uchumi wa Tanzania na lazima watu wenye msuli mkubwa wa kifedha, utaalamu na uendeshaji lazima watafutwe ili kusaidia uendeshaji.
Amesema pia kumekuwepo na wizi na kupungua kwa ufanisi bandarini, hivyo lazima wawekezaji wenye uwezo mkubwa wa udhibiti wapewe fursa kuendesha bandari.
Chanzo: Msemaji Mkuu wa Serikali (Clubhouse)