JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kwa data ipi? au mathematical model ipi kutoa conclusion kama hiyo? Tunataka atuwekee investigator's brochure tuone hiyo data
Kutoka Morogoro, Viwanja vya Shule ya Moro Sec katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, ITV imezungumza na Dk. Jerome Kamwela ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TACAIDS anasema:
"Kama tumebakiza miaka 7 kutokomeza UKIMWI, maana yake kati ya leo mpaka 2030 miaka 7 tu imebaki, maana yake huduma zipo, uelewa upo, lakini tujue maambukizi mapya yanatokea kwenye jamii."
Chanzo: ITV
N kweliZile rapid tests zikianza kupatikana na kununuliwa kwa wingi kama vipimo vya mimba nitajua uelewa umeongezeka na hiyo 2030 tutafikia hilo lengo.
Kinyume na hapo ni kusubiri tu upikwaji wa takwimu baada ya 2030!
Hujaelewa hawa jamaa, wao wanaweka ngonjera kwenye mambo yanayohitaji umakini mkubwaMbona maambukizi bado yapo kwa kasi UKIMWI utatokomezwaje baada ya miaka 7?
Haya Madawa yanatengenezwa under copyright je wenyewe wakiamua kupiga marufuku utengenezaji?Hujaelewa hawa jamaa, wao wanaweka ngonjera kwenye mambo yanayohitaji umakini mkubwa
Yaani wanaposema kutokomeza ukimwi wanaamaanisha ile hali ya mtu mwenye HIV kuishi tu na maamhukizi pasipo kuugua magonjwa yanayatokana na upungufu wa kinga, au kwa kifupi kumudu kudhibiti asifikie upungufu wa kinga
Lakini kwa upande wa pili hii si hatua ya kujisifu ikiwa maambukizi yanaendela kutokea. Ni hali hatarishi kwa sababu hata hiyo kuweza kudhibiti upungufu wa kinga usitokee kwa kutumia dawa hatufanyi kwa uwezo wetu, sasa itakuwaje siku moja wanaofadhili hizi dawa wakishindwa kuendelea kuzileta
Kama tumeshindwa malaria kweli ukimwi tutauweza?Mbona ukimwi umebaki Afrika tu? Ulaya na amerika wanahangaika na mengine.
Serikali ziwe makini