Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Michezo , Ally Mayai atembelea Uwanja wa Benjamin Mkapa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ndio Taarifa mpya iliyosambazwa na Wizara ya Michezo nchini Tanzania , kwamba Kaimu Mkurugenzi mpya wa idara ya michezo , Mh Ally Mayai , ametembelea ofisi ndogo ya kitengo chake Mjini DSM , na baadaye akatembelea Uwanja wa Mkapa kujionea hali halisi ya uwanja huo na changamoto zake .

Tunamtakia kila la heri kwenye majukumu yake mapya .
 
Rafiki mayai tembele

Sio mtu mzuri connection zinamdondokea Sana

1---kaimu meneja uwanja yeye

2---afsa masoko mwalimu nyerere airport yeye

Uchambuzi yeye
 
Yeah, Form Six alipata division zero, ila mi namtetea maana alikuwa busy na soka, shule akaiweka kando. Lakini alishtuka akastaafu soka akiwa bado kijana, akaenda chuo kuanza na Certificate, ambayo ilimpeleka mbele zaidi hadi Higher Education
Shule gani, level na combination ipi alipata sufuri?
 
Yeah, Form Six alipata division zero, ila mi namtetea maana alikuwa busy na soka, shule akaiweka kando. Lakini alishtuka akastaafu soka akiwa bado kijana, akaenda chuo kuanza na Certificate, ambayo ilimpeleka mbele zaidi hadi Higher Education
Sasa mbona umeshikilia tu alipata zero wakati kumbe alisahihisha makosa na kupata mpaka elimu ya juu? Kwa sasa ameshakaa vizuri kielimu hatutakiwi kuangalia makosa ya nyuma ambayo ameshayarekebisha.

Kuna jamaa yangu mmoja ni Profesa mbobevu na ni Mkuu wa Chuo kimajawapo kikubwa nchini ila alipata Div 4 kidato cha nne akaenda ualimu vyuo vya Diploma akafundisha baadae akaenda degree kisha Masters USA na akapiga na PhD baadae akawa Prof. Sasa hapo unakuja mtu kama wewe unasema Prof alipata Div 4 huko nyuma ina madhara gani wakati alishajisahihisha?

Tuache husda na chuki kwa watu wenye mafanikio. Tuchukue kama funzo ili na sisi turekebishe tulipokosea katika njia za kuelekea mafanikio
 
Huyo atakuwa profesa Anangisye???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…