Kairuki ataka ushirikiano kuukabili unyanyasaji
"Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha vitendo hivi vinatokomezwa." Angellah Kairuki.
KWA UFUPI
- Rai hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki
- wakati akizindua siku 16 za kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.
Asema endapo wananchi watashirikiana na Serikali vitendo hivyo vinaweza kutokomezwa nchini.
Dar es Salaam. Washiriki mbalimbali wa maendeleo na wadau wa masuala ya jinsia wametakiwa kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia vinafikia tamati.
Rai hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki wakati akizindua siku 16 za kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.
Sambamba na uzinduzi huo Kairuki alizindua pia mfumo wa utoaji wa huduma kwa mfumo wa One Stop Center ambao unajumuisha huduma zote muhimu kwa watakaokutana na ukatili wa kijinsia kama vile polisi, afya na ustawi wa jamii kutolewa sehemu moja.
Alisema licha ya kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikiongezeka kila kukicha, ni asilimia 4 tu ya kesi hizo ndiyo huripotiwa katika vyombo vya sheria hali inayochangia wahusika kuendelea kuwa huru mitaani.
"Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha vitendo hivi vinatokomezwa, lakini wanawake ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo wamekuwa wakinyanyasika hawakimbilii kutafuta msaada wa kisheria" alisema Kairuki.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF), Naomi Kaihura alisema licha ya kuwepo kwa jitihada mbalimbali za kupinga vita vitendo vya ukatili, changamoto kubwa inabaki katika upatikanaji wa fomu za polisi ambazo hutoa kibali kwa muathirika kupata matibabu.
Alisema hali hiyo kwa kiasi kikubwa inachangia waathirika kupoteza maisha na wengine kukata tamaa ya kutoa ripoti kuhusiana na ukatili waliofanyiwa.
"Ukiritimba katika upatikanaji wa PF3 ni changamoto kubwa hali inayosababisha waathirika kupoteza maisha hata kabla hawajapata matibabu," alisema. Kairuki ataka ushirikiano kuukabili unyanyasaji - Kitaifa - mwananchi.co.tz
Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha vitendo hivi vinatokomezwa. Angellah Kairuki.
KWA UFUPI
- Rai hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki
- wakati akizindua siku 16 za kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.
Asema endapo wananchi watashirikiana na Serikali vitendo hivyo vinaweza kutokomezwa nchini.
Dar es Salaam. Washiriki mbalimbali wa maendeleo na wadau wa masuala ya jinsia wametakiwa kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia vinafikia tamati.
Rai hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki wakati akizindua siku 16 za kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.
Sambamba na uzinduzi huo Kairuki alizindua pia mfumo wa utoaji wa huduma kwa mfumo wa One Stop Center ambao unajumuisha huduma zote muhimu kwa watakaokutana na ukatili wa kijinsia kama vile polisi, afya na ustawi wa jamii kutolewa sehemu moja.
Alisema licha ya kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikiongezeka kila kukicha, ni asilimia 4 tu ya kesi hizo ndiyo huripotiwa katika vyombo vya sheria hali inayochangia wahusika kuendelea kuwa huru mitaani.
Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha vitendo hivi vinatokomezwa, lakini wanawake ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo wamekuwa wakinyanyasika hawakimbilii kutafuta msaada wa kisheria alisema Kairuki.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF), Naomi Kaihura alisema licha ya kuwepo kwa jitihada mbalimbali za kupinga vita vitendo vya ukatili, changamoto kubwa inabaki katika upatikanaji wa fomu za polisi ambazo hutoa kibali kwa muathirika kupata matibabu.
Alisema hali hiyo kwa kiasi kikubwa inachangia waathirika kupoteza maisha na wengine kukata tamaa ya kutoa ripoti kuhusiana na ukatili waliofanyiwa.
Ukiritimba katika upatikanaji wa PF3 ni changamoto kubwa hali inayosababisha waathirika kupoteza maisha hata kabla hawajapata matibabu, alisema. Kairuki ataka ushirikiano kuukabili unyanyasaji - Kitaifa - mwananchi.co.tz
Watuambie aliyebaka Mtoto wa Miaka 14 wamemfanya nini wasisumbue wananchi kwa maelezo marefu yasiyo nakichwa wala miguu.
Sheria iko wazi wao wanapiga chenga kwenye media tumechoka na hayo mawito yao tunataka utekelezaji wa haya yafuatayo.
1.Atuambie ni kwanini sheria kandamiza zinazobagua wana wake bado zinaendelea kutambulika na kutumika
2.Anaifahamu Ripoti ya Nyalali wao Kama serikali wamefanya nini?
3.Kabla ya huu mfumo wa one stop centre kulikuwa na mfumo wa Dawati la Jinsia ambao kimsingi haukusaidia lolote zaidi ya kujigeuza kitengo cha kupiga danadana na kuwalinda wahalifu hasa vigogo na mfumo huo ulikuwa bado hauja enea nchi nzima sasa wanarukia mfumo huu mpya wakati maafisa ustawi wajamii ni wachache kupindukia na hata hao waliopo wamepigika na hawana moral ya kazi anatueleza nini kuhusu umuhimu wa mfumo huu na wamejifunza nini kutokana na kutotilia maanani mfumo wa Dawati la jinsia.
Baaada ya kutu fahamisha kuhusu hayo ndo atoe wito kwetu vingenevyo statement zao do remain useless as a toothless bulldog