Kaisari Agusto mtawala wa kwanza wa himaya ya Roma na kuzaliwa kwa Kristo

Kaisari Agusto mtawala wa kwanza wa himaya ya Roma na kuzaliwa kwa Kristo

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
13,628
Reaction score
20,992
Danieli 11:20 Ndipo badala yake atasimama mmoja, atakayepitisha mwenye kutoza ushuru kati ya utukufu wa ufalme wake; lakini katika muda wa siku chache ataangamizwa, si kwa hasira, wala si katika vita.

Baada ya vita vya Actium 31 K.K ambavyo vilimpa ushindi Octavian dhidi ya Mark Antony na Kleopatra, hatimaye himaya ya Roma ikawa chini ya mamlaka ya mtawala mmoja mwaka 27 K.K. Kuinuka kwa Octavian katika enzi ya Roma kuliashiria mwisho dhahiri wa Jamhuri ya Kirumi. Mnamo 27 KK Octavian aliitwa Augustus na Seneti, na akapewa mamlaka ambayo haijawahi kutokea. Augustus inamaanisha “mtukufu au mungu”. Katika kipindi cha utawala wake wa miaka 45, Augusto alikamilisha mabadiliko ya Roma kutoka jamhuri hadi ufalme. Kwa miaka 500 iliyofuata, Roma ingekuwa udikteta wa kijeshi, unaotawaliwa na mtawala (imperator). Mwezi wa 8 aliuita “Augusto” kwa jina lake kama ulivyo mwezi wa 7 uliobeba jina la Kaisari Julius, yote hayo alitaka kuonekana kuwa mkuu kama mtangulizi wake. Octovian akawa mtawala wa kwanza wa himaya ya Roma na kuendeleza mikakati ya mjomba wake, na huyu alikuja na mikakati kabambe ya kukusanya kodi na akaifanya Roma kuwa tajiri sana, zama zake zinaitwa zama za dhahabu. Hata Wayahudi walitumia mbinu za kumtega Yesu kwa kodi ya Kaisari. (Mathayo 22:17). Katika wakati wa utawala wake tunasoma katika Luka 2:1-7

“Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu. Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa liwali wa Shamu. Watu wote wakaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao. Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi; ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba. Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia, akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.”

Sheria za kodi zinawaleta wazazi wa Kristo Bethlehemu na hapo ndipo mwana wa Mungu alizaliwa. Kaisari Augusto ambaye alijiona mungu sasa hufanywa kuwa wakala wa kutimiza malengo ya Mungu wa mbinguni. Huu ndio wakati ambapo utukufu wa ufalme wa Mungu ulipangwa kuletwa ulimwenguni. Kristo, Mfalme wa wafalme na Bwana wa Bwana yu karibu kuzaliwa, Mwokozi wa wanadamu wote. Mkuu wa ulimwengu wote akaja ulimwenguni kama mtoto mchanga. Tamko la mtawala wa Kirumi kuhusu kuandikishwa kwa watu walio katika utawala wake lilikuwa limefika hadi kwa wakazi wa vilima vya Galilaya. Kama ilivyokuwa zamani kwa Koreshi aliyeitwa kukalia kiti cha enzi cha himaya ya ulimwengu ili awaweke huru mateka wa Bwana. Kaisari Augusto naye anafanywa wakala kwa ajili ya utimilifu wa kusudi la Mungu kwa kumleta mama wa Yesu Bethlehemu.

Huyo mama ni wa ukoo wa Daudi, na lazima Mwana wa Daudi azaliwe katika mji wa Daudi. Kutoka Bethlehemu, alisema nabii, “atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele." Mika 5:2. Hapo Bethlehemu katika hori la kulishia wanyama ndipo Mkombozi wa ulimwengu anapozaliwa. Kisa cha Bethlehem ni mada isiyoweza kuelezwa ikaisha yote. Ndani yake kumefichwa "utajiri na hekima na maarifa ya Mungu!” Rom. 11:33. Tunashangazwa na kafara ya Mwokozi ya kufanya mbadilishano kwa kuchukua hori la ng’ombe badala ya kiti cha enzi cha mbinguni, na badala ya wingi wa malaika wamzungukao akawa na wanyama katika kibanda. Kiburi cha mwanadamu na kutaka kujitosheleza vinakemewa na uwepo wa Mwokozi.

Sasa Mkuu halisi wa Ulimwengu dhidi ya mkuu wa muda wa dunia Kaisari Agusto, wote wanadai umungu, lakini leo Kristo anaishi, na yule mkuu wa Roma leo ni marehemu. Biblia inatuambia kuhusu mtu huyu ambaye aliufanya Ufalme wa Kirumi kuwa na nguvu nyingi, ni kwamba alikuwa mtozaji wa kodi, wakati ufalme wake ulipokuwa katika utukufu, na kwamba baada ya kutawala kwa miaka 45, alimaliza kazi yake kwa kifo cha kupewa sumu na mauti imemshikilia hadi leo. Lakini Kristo alimaliza kazi yake kwa kifo cha msalaba, kifo cha ushindi dhidi ya dhambi na shetani.

Sauti yake ya mwisho msalabani “imekwisha” ilibadilisha historia ya dunia, “Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi. (Yohana 19:30, Mathayo 27:51-53). Na baada ya siku tatu, alifufuka kwa ushindi mkuu, “Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee. Waebrania 7:25.
 
Cizar ......aliyepigana na Spartacus na kuwashinda .....ndiye ninayemuona ni kiboko sana
 
Danieli 11:20 Ndipo badala yake atasimama mmoja, atakayepitisha mwenye kutoza ushuru kati ya utukufu wa ufalme wake; lakini katika muda wa siku chache ataangamizwa, si kwa hasira, wala si katika vita.

Baada ya vita vya Actium 31 K.K ambavyo vilimpa ushindi Octavian dhidi ya Mark Antony na Kleopatra, hatimaye himaya ya Roma ikawa chini ya mamlaka ya mtawala mmoja mwaka 27 K.K. Kuinuka kwa Octavian katika enzi ya Roma kuliashiria mwisho dhahiri wa Jamhuri ya Kirumi. Mnamo 27 KK Octavian aliitwa Augustus na Seneti, na akapewa mamlaka ambayo haijawahi kutokea. Augustus inamaanisha “mtukufu au mungu”. Katika kipindi cha utawala wake wa miaka 45, Augusto alikamilisha mabadiliko ya Roma kutoka jamhuri hadi ufalme. Kwa miaka 500 iliyofuata, Roma ingekuwa udikteta wa kijeshi, unaotawaliwa na mtawala (imperator). Mwezi wa 8 aliuita “Augusto” kwa jina lake kama ulivyo mwezi wa 7 uliobeba jina la Kaisari Julius, yote hayo alitaka kuonekana kuwa mkuu kama mtangulizi wake. Octovian akawa mtawala wa kwanza wa himaya ya Roma na kuendeleza mikakati ya mjomba wake, na huyu alikuja na mikakati kabambe ya kukusanya kodi na akaifanya Roma kuwa tajiri sana, zama zake zinaitwa zama za dhahabu. Hata Wayahudi walitumia mbinu za kumtega Yesu kwa kodi ya Kaisari. (Mathayo 22:17). Katika wakati wa utawala wake tunasoma katika Luka 2:1-7

“Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu. Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa liwali wa Shamu. Watu wote wakaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao. Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi; ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba. Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia, akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.”

Sheria za kodi zinawaleta wazazi wa Kristo Bethlehemu na hapo ndipo mwana wa Mungu alizaliwa. Kaisari Augusto ambaye alijiona mungu sasa hufanywa kuwa wakala wa kutimiza malengo ya Mungu wa mbinguni. Huu ndio wakati ambapo utukufu wa ufalme wa Mungu ulipangwa kuletwa ulimwenguni. Kristo, Mfalme wa wafalme na Bwana wa Bwana yu karibu kuzaliwa, Mwokozi wa wanadamu wote. Mkuu wa ulimwengu wote akaja ulimwenguni kama mtoto mchanga. Tamko la mtawala wa Kirumi kuhusu kuandikishwa kwa watu walio katika utawala wake lilikuwa limefika hadi kwa wakazi wa vilima vya Galilaya. Kama ilivyokuwa zamani kwa Koreshi aliyeitwa kukalia kiti cha enzi cha himaya ya ulimwengu ili awaweke huru mateka wa Bwana. Kaisari Augusto naye anafanywa wakala kwa ajili ya utimilifu wa kusudi la Mungu kwa kumleta mama wa Yesu Bethlehemu. Huyo mama ni wa ukoo wa Daudi, na lazima Mwana wa Daudi azaliwe katika mji wa Daudi. Kutoka Bethlehemu, alisema nabii, “atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele." Mika 5:2. Hapo Bethlehemu katika hori la kulishia wanyama ndipo Mkombozi wa ulimwengu anapozaliwa. Kisa cha Bethlehem ni mada isiyoweza kuelezwa ikaisha yote. Ndani yake kumefichwa "utajiri na hekima na maarifa ya Mungu!” Rom. 11:33. Tunashangazwa na kafara ya Mwokozi ya kufanya mbadilishano kwa kuchukua hori la ng’ombe badala ya kiti cha enzi cha mbinguni, na badala ya wingi wa malaika wamzungukao akawa na wanyama katika kibanda. Kiburi cha mwanadamu na kutaka kujitosheleza vinakemewa na uwepo wa Mwokozi.

Sasa Mkuu halisi wa Ulimwengu dhidi ya mkuu wa muda wa dunia Kaisari Agusto, wote wanadai umungu, lakini leo Kristo anaishi, na yule mkuu wa Roma leo ni marehemu. Biblia inatuambia kuhusu mtu huyu ambaye aliufanya Ufalme wa Kirumi kuwa na nguvu nyingi, ni kwamba alikuwa mtozaji wa kodi, wakati ufalme wake ulipokuwa katika utukufu, na kwamba baada ya kutawala kwa miaka 45, alimaliza kazi yake kwa kifo cha kupewa sumu na mauti imemshikilia hadi leo. Lakini Kristo alimaliza kazi yake kwa kifo cha msalaba, kifo cha ushindi dhidi ya dhambi na shetani. Sauti yake ya mwisho msalabani “imekwisha” ilibadilisha historia ya dunia, “Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi. (Yohana 19:30, Mathayo 27:51-53). Na baada ya siku tatu, alifufuka kwa ushindi mkuu, “Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee. Waebrania 7:25.

Ukristo na biblia inahitaji utulivu wa akili ili uuelewe! ukibeba nadharia za mwili ukaacha nadharia za roho huwezi uelewa hata usomewe biblia yote mara elfu na ndio sababu kubwa wasio elewa huishia kuutusi tu
 
Hoja yako Ni ipi ndugu,sijakuelewa
 
Ahueni mpaka sasa sijaona Wapinga Kristo wakija kufanya vurugu na kufuru kwenye huu uzi. Ubarikiwe sana Mtumishi wa Mungu kwa historia nzuri.

Na kwa wale wasio ifahamu historia kwa kina, ni kwamba Dola ya Kirumi ndiyo Dola maarufu kabisa duniani kutekeleza vitendo vya utumwa (Slavery) katika sehemu kubwa ya dunia kuanzia miaka zaidi ya 3000 huko BC mpaka kwenye karne ya tano (400 AD).
 
Mnamfahamu Kinjekitike Ngwale, Kabaka Mutesa, Mkwawa, Ole Lenana n.k?
 
Historia Iko sahihi sana. Wakristo sasa amkeni msome historia ya falme zilizotangulia na pia soma historia ya kanisa

Wale walokole wenzangu ndio nawasisitiza zaidi maana wengi ni weupe sana kwenye kusoma neno la Mungu na kujifunza zaidi kuhusu imani yetu ndani ya Kristo Yesu pamoja na historia ya kanisa kwa ujumla.

Ubarikiwe mleta mada.
 
Back
Top Bottom