Kajala na Harmonize wameachana? Kajala afuta picha za Harmonize Instagram na kumu–unfollow

Kajala na Harmonize wameachana? Kajala afuta picha za Harmonize Instagram na kumu–unfollow

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Moja kati ya taarifa inayo-trend kwa sasa mitandaoni ni kuhusu msanii wa filamu Kajala Masanja na msanii wa muziki Harmonize ambao inasemekana penzi lao limefika mwisho kutokana na baadhi ya viashiria vya mazingira vilivyojitokeza.

HAMO-KAJALA.png

Taarifa hiyo imekuja baada ya Kajala Masanja kufuta picha zote alizowahi ku-post akiwa na Harmonize kwenye mtandao wa Instagram kisha kumu-unfollow kwenye mtandao na kuandika ujumbe wa Kiingereza uliotafsirika kama

Usimuumize mtu kwa ajili ya sababu zako binafsi

Mahusiano ya Harmonize na Kajala yalikuja kwa kasi na yalivutia watu wengi hadi kufikia hatua ya kuchorana tattoo japo baadhi ya watu wengine walikuwa wanalipinga penzi lao mitandaoni.
 
Muuza nyapu alikutana na mtengeneza kiki, wakapatana kibiashara. Biashara imeshafanyika, sasa kila mtu anaendelea na maisha yake.
Yamebakia mazuzu tu mitaani kufuatilia maisha yao mitandaoni.
😂 😂 😂
 
Meat in one community, Poison in another and vice versa.
 
Back
Top Bottom