Kajala: Wema ni mnafki

Kajala: Wema ni mnafki

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
STAA wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja ameibuka na kusema kuwa ushosti wake na Miss Tanzania 2006 /07, Wema Sepetu , uliorudishwa hivi karibuni baada ya kuwekana sawa ni wa kinafiki huku akidai Wema ni kigeugeu .

Staa wa filamu za Kibongo , Kajala Masanja Akizungumza kwa kujiamini mbele ya waandishi wetu, juzi Jumatano pande wa Mikocheni jijini Dar es Salaam, Kajala alisema : "Wema ni mnafiki kabisa . Upatanisho wetu ni wa uongo .

Mimi moyoni nimeondoa kinyongo lakini mwenzangu naona kama bado ana donge moyoni. " Kajala alisema hayo alipoulizwa na Risasi Jumamosi , sababu ya kutoonekana kwenye tukio la futari lililofanyika nyumbani kwa mama mzazi wa Mbongo Fleva , Nasibu Abdul ' Diamond ' , Sanura Kassim ambaye ni mkwe wa shosti wake huyo.

Katika tukio hilo, mama Diamond alifanyiwa sapraizi ya nguvu alipokabidhiwa gari kali aina ya Toyota Lexus Harrier kama zawadi ya bethidei yake , ambayo ilitolewa na meneja wa Diamond , Babu Tale kwa niaba ya mwanamuziki huyo ambaye alikuwa safarini nchini Marekani .

"Tunakubaliana kuwa kitu kimoja lakini mwenzangu anaonekana ana kinyongo. Hebu angalia, anawezaje kuacha kunialika kwenye shughuli muhimu kama ile kama kweli tumepatana? Mbona amealika watu wengi lakini mimi ameniacha ? Wema aache unafiki bwana.

"Mbaya zaidi , hivi juzi tu ameweka picha ya msichana mmoja anayekaa China, huyu mdada anaitwa Sabrina , niliwahi kugomabana naye , lakini yeye amemuweka Instagram na kumwandikia maneno kibao ya kumsifia akim- wish happy birthday, hapo si kama ananisimanga ? Wema si mkweli , " alisema Kajala .

Akizungumzia ishu hiyo , siku ya tukio Wema alisema : "Ukiniuliza kuhusu Kajala kutokuwepo hapa , kwa kweli utakuwa kama unanichanganya tu maana leo sijashika simu muda mrefu sana. "Hata ujio wangu hapa nilikurupushwa , ndiyo maana sijakumbuka kumuita Kajala , lakini tuko vizuri na mara ya mwisho tumeongea jana ( Jumapili ) usiku tu , " alisema Wema .
 
binamu yaani kuna jambo nimelisikia acha tu mie hoi.. hawa maselebuliti balaa
 
Hahaha duh ila hata kama wamesameheana si lazima waendelee kuwa marafiki kila mtu ni vyema ashike ustaarab wake
 
Hivi mmewahi kusikia masupastaa wa kike wa mbele wakiwa na ushoga kama huu wa bongo wa kufatana kama kumbikumbi hadi chooni? ukosefu wa kazi za kufanya na kuishia kusubiri pesa rahisi rahisi no matter what......wanazidiwa hata na wadada wa vijijini wasio na elimu wala uelewa mpana lakini wanashinda mashambani ........
 
Wema naye kufulia kumempanikisha tu sasa hivi kama sio domo hasikii na wema aachane na ushosti haumsaidii lolote
 
Kula like kumiii
 
Kwa wanawake kuchukiana ni kitu cha kawaida
 
Hivi mmewahi kusikia masupastaa wa kike wa mbele wakiwa na ushoga kama huu wa bongo wa kufatana kama kumbikumbi hadi chooni? ukosefu wa kazi za kufanya na kuishia kusubiri pesa rahisi rahisi no matter what......wanazidiwa hata na wadada wa vijijini wasio na elimu wala uelewa mpana lakini wanashinda mashambani ........

Wenzao wakina rihhana mambo ya ushoga sijui kucheza vigodor wao hawana, Ushoga wa mastaa wa bongo ni umbea,uchonganishi,kuibiana mabwana na uchawi pamoja na kurogana

Naona kamis kubeba mapochi, amwachie cheusi dawa bhna ye si alichezea bahati, mama ubaya hatak shobo sasa ivi
 
Wema naye kufulia kumempanikisha tu sasa hivi kama sio domo hasikii na wema aachane na ushosti haumsaidii lolote

Wema aache mashoga si atakufa yule anavyopenda umbea, uboss uchwara wa kubebewa mapochi na kucheza vigodoro
 
Back
Top Bottom