Kaka Mwigulu Tozo ya kibenki ni Ujambazi, hamia 10% Kodi ya Nyumba

Kaka Mwigulu Tozo ya kibenki ni Ujambazi, hamia 10% Kodi ya Nyumba

Mwanamwaiche

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2022
Posts
665
Reaction score
968
Sina mengi ujumbe uko wazi Singida Big Stars ni mfano wa hizo apartments za madolari, acha kulia Kwa uhuni wenu jikite na hoja, akili za kitozo tozo ni uzuzu, toa hata arguments za kiakili et ooh tozo ni maoni ya wananchi, ujinga wa kizuzu double taxation ni ya wananchi wa kawaida?

Mbona hoja yako inahusu laki3 ya mshahara Kwa hio wafanyakazi ndio wamekushauri wawe double taxed?

Akili za wizi na uzuzu heshimuni hio dhamana. Ni upumbavu mkipewa dhamana mnajiona mshakuwa malaika.

Huu uchizi unakuja na gari ya million 500 halafu unatokea mfano wa apartments, Anza na kubana matumizi, unakuwaje waziri wa fedha asiehimiza punguzo au kubana matumizi yasiyo ya lazima au yasiyo tija, au yalioyo juu yako kibajeti.

Tumieni akili kuna vibwengo wengi kwenye mataasisi na idara mmewapa magari ma VX, V8.

Care with collective pains and thinking. We expected leaders to starve at the expense of state ecomic health and prosperity.

Think of expenditure first before revenue collection
 
Watanzania, tufanyeni kazi, kazi. Unapolaumu serikali ipe na maoni na namna yakuendesha serikali. Siyo kulaumu na kutukana viongozi tu.
 
Watanzania, tufanyeni kazi, kazi. Unapolaumu serikali ipe na maoni na namna yakuendesha serikali. Siyo kulaumu na kutukana viongozi tu.
Serikali inayosubiri maoni ya wananchi juu ya namna bora ya kuendesha nchi bila kurudisha nyuma maendeleo ya watu wake haifai kuongoza nchi.
 
Serekali ifahamu hayo mabanda ndiyo yanayosomesha vijukuu na hata rangi kupigika inashindikana,bili za maji umeme zikija ni balaa tupu hazilipiki, familia za kibantu kama mnavyozifahamu,na ajira hakuna,tabu kweli unga umepanda,maana uswazi ni mwendo wa ugali tu,hakuna wali huku.
 
Mwigulu anasahau kuwa wananchi wanalipa kodi huku wao wakitunga sheria na wakishatunga sheria wao wanaona ni lazima watu wailipe hata kama ina mapungufu na pia inatakiwa wajipime kama Bunge ni la Wananchi wao wamepitisha harafu wananchi wanaipinga maana yake hata hilo Bunge halina kazi yeyote zaidi ya kutafuna kodi za Wananchi kama wanapitisha vitu vya hovyo hovyo kila mara..
 
Watanzania, tufanyeni kazi, kazi. Unapolaumu serikali ipe na maoni na namna yakuendesha serikali. Siyo kulaumu na kutukana viongozi tu.

MTOA MADA KATOA HUU USHAURI

Huu uchizi unakuja na gari ya million 500 halafu unatokea mfano wa apartments, Anza na kubana matumizi, unakuwaje waziri wa fedha asiehimiza punguzo au kubana matumizi yasiyo ya lazima au yasiyo tija, au yalioyo juu yako kibajeti.

unaoweza ona tusi, kumbe ndio sifa anayo staili mtu.
 
Mwanasiasa ajae akizungumzia tu kuondoa tozo amepita huyo bila pingamizi, kama kuna njama ..Fulani Fulani vile!
 
Mtu anaenda na gari la 450m kuomba watu wenye nyumba za 10m walipe kodi za wapangaji wao na kutoza kodi na pia ukitoa kiasi chochote bank wanakutoza kodi kwa hela iliyokatwa kodi za kutosha unaiweka ili ifanye mzunguko mwingine wa kikodi kutoka tuu huko ambako hujapata faida yeyote zaidi ya makato ya bank charges kwa kukutunzia fedha nao Serikali inakata Tozo kwa wewe kuweka hela bank hawa sijui wachumi wa wapi hawa badala ya kuanza kubana matumizi anataka kuwakandamiza wananchi bila kuwa na hoja zenye mashiko..
 
Back
Top Bottom