SoC02 Kaka Shabani ni wa kuigwa

SoC02 Kaka Shabani ni wa kuigwa

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 15, 2022
Posts
5
Reaction score
0
Kaka Shabani, ni kijana mwenye historia ndefu na ya kipekee katika maisha yetu ya siku hizi. Huyu ni mkaka anayemiliki pikipiki zipatazo ishirini na tano na viwanja katika maeneo mbalimbali, katika hali isiyo ya kawaida siku moja ilimlazimu atoe historia yake kutokana na tuhuma na hujuma mbalimbali zinazohusiana na imani mbalimbali za kishirikina juu ya mali zake anazozimiliki.

Kiukweli siyo jambo la kawaida sana katika maisha yetu ya kitanzania kwa kijana mwenye umri chini ya miaka thelathini kuwa na mali kiasi kama hicho, hivyo watu wengi katika jamii iliyo mzunguka walianza kupata wasiwasi juu ya umiliki wa mali zake, jambo hili lilipekea kaka huyu kutuhumiwa na kuhisiwa na kesi kama vile ukoperaji na utoaji wa kafara vilevile kuna wengine walifikia kusema kwamba yule kijana amejiunga na freemason.

Hali au fikra hii iliendelea kukua zaidi katika jamii kila siku zinavyozidi kwenda kutokana na maendeleo ya kaka huyo yaliyokuwa yakionekana siku hadi siku. Maendeleo ya kaka Shabani yalizidi kuonekana baada ya idadi ya pikipiki zake kuzidi kuenea katika maeneo jirani na kitongoji anachoishi, ikumbukwe kadiri maendeleo ya kaka shabani yanavyozidi kuonekana hivyohivyo fikra mbaya na potofu zilizidi kuota mizizi katika jamii. Siku moja katika kijiji jirani walifika kundi la waganga wa kienyeji ambao ilisemekana wanatoa uchawi na ukoperaji . Watu wa kijiji ambacho kaka shabani anaishi wakaamua kuwaleta wale waganga katika kijiji hicho ambacho kaka Shabani anaishi humo ili waje kuondoka uchawi na ukoperaji wa kaka Shabani.

Kaka Shabani alipoambiwa kuhusu ujio wa waganga hao na lengo lao hilo, kwasababu waganga wale walihitaji kuja hadi ndani ya nyumba ya kaka Shabani, kaka huyu akawaambia amna tatizo nyie mtaingia tu ndani kwasababu mmesema huo uchawi wangu nimeuweka ndani basi nyie mtaingia tu, lakini aliwapa mashariti mawili makubwa, shariti hilo lilikuwa kwamba kwasababu nyie mmesema kwamba uchawi upo humu ndani kwangu, basi hakikisheni mnaupata na mnatoka nao nje kila mtu auone, lakini pia aliwaambia wasiingie na mfuko wowote ambao wangeweza kuweka kitu ndani ya mfuko huo ambao wangeweza kumgeukia na kusema kitu hicho wamekikuta ndani ya nyumba ya kaka Shabani.

Bila ya kupoteza muda, waganga wale walishindwa na mashariti yale mawili ya kaka Shabani na wakaamua warudi kijini walichotokea, watu wengi walilaumu kwanini wale waganga wameamua kuachana na Shabani wakati yule kijana ndio anatukopera sisi, lakini kutokana na kushindikana kwa njia ya udanganyifu ambao wale waganga wangeufanya ili kuthibitisha kwamba kaka Shabani ni mkoperaji waliamua kuachana na kaka huyo.

Kutokana na maudhi na kero kubwa ambayo Shabani aliivumilia kwa muda mrefu, siku moja maskani katika wataki wa jioni vijana wakiwa wamepumzika baada ya shughuli za mchana kutwa, maskani pale palianzishwa stori za kizushi na chokochoko kuhusu utajiri na umiliki wa mali, jambo hili liliwagawa watu katika makundi mawili, kundi la kwanza walikuwa wakiamini vijana wengi hupata mali kwa kutoa kafara na ukoperaji na kundi la watu wa chache walikuwa ndio waumini wa kufanya kazi kwa bidii na kumtegemea Mungu. Kaka Shabani alikaa kimya ili kuwasikiliza wakiminyana na kubishana lakini kila kundi lilikuwa na hoja zake, waumini wa kafara na ukoperaji walishikilia kauli yao ya kwamba mbona sisi tunafanya kazi lakini hatupati mali nyingi kiasi cha kuitwa matajiri?

Punde, mmoja kati ya wafuasi wa kufanya kazi na kumuamini Mungu akasema " nyie ndio maana mnasema Shabani mchawi ,mara anakopera ,kumbe nyinyi wavivu ampendi kazi na mnapenda raha" hapo ndipo Shabani na yeye akaanza kupata hamu yakuwaelezea kivipi alipata utajiri wake.

Shabani alianza kwa kusema, " mwajua nyie hebu nisikilizeni, nyie mnasema watu wachawi wanakopera na vitu kama hivyo, lakini mnajua mimi nimeanzia wapi au mnaongea tu, mimi nimeanzia kuendesha pikipiki ya mjomba, fekon ile ya mjomba nimeanza kuitumia mimi, nilikuwa kila asubuhi lazima nikamchotee maji ya ng'ombe wake na maji ya nyumbani kwake, kumbukeni hapo mafuta yangu na hela ya maji pia nalipia mimi mwenyewe.

Nikimaliza kuchota maji naingia mtaani kubeba abiria na mizigo ya aina mbalimbali kama vile magunia ya nazi, mizigo ya dukani, miwa na vitu kama hivyo, lakini pia mjomba akiwa na safari nampeleka na pikipiki mafuta nalipia mimi mwenyewe, nampeleka mjomba na namrudisha nyumbani kwake, lakini muda huo wote hela zangu nilikuwa naweka mpaka nikapta pesa ya kununua pikipiki yangu.

Nikamrudishia mjomba pikipiki yake nikaendelea na kazi na pikipiki yangu, nilikuwa nabeba abiria muda wowote nitakaopigiwa simu hata saa tisa za usiku, na siku zote nilikuwa naamka mapema ili niwahi abiria, nikapambana mpaka nikanunua pikipiki yangu ya pili huo ulikuwa mwaka 2014, pikipiki mpya nikabaki nayo mwenyewe ile niliyokuwa natumia nikampa kijana afanyie kazi, kwa siku alikuwa ananipa elfu kumi.

Hivyo hivyo nikawa napambana muda wengine abiria amna nafanya kazi za kulima vibarua, waulize wakina bwana maendeleo na Mnyeheri, mimi ndio nilikuwa mkibarua wao mkubwa, nilikuwa nalima hekari moja peke yangu kwa siku tatu, nikitoka nyumbani saa kumi na moja kasoro asubuhi narudi saa nane mchana, kumbukeni nilima vibarua na pikipiki nilikuwa nazo mbili.

Hivyo hivyo nakumbuka mwaka 2014 huohuo walikuja watu wanatafuta watu wakupiga zege kwenye majengo mapya ya halmashauri, nakumbuka kama kesho ndio sikukuu ya Idi na leo ndio watu wanatafutwa, nyote nyie mlikataa mimi peke yangu ndio nilienda kupiga zege siku ile, nakumbuka nikirudi hapa saa nne usiku nikatafuta chakula nikala nikaingia ndani nikalala, saa kumi na moja alfajiri nikachukua baiskeli nikaenda tena kupiga zege, niwaulize nyie, wewe ungekuwa una pikipiki mbili ungeenda kupiga zege?

Lakini mimi nilikuwa naenda kupiga zege na watu wala walikuwa hawajui kama nina pikipiki mbili, siku hizo hakuna aliyekuwa anajua kwamba mimi natembea na mdada gani, nakula mihogo ya kukaanga ndio ilikuwa chai yangu, yani nilikuwa na bajeti kali, nilikuwa navaa nguo za mtumbani na pia nilikuwa na nguo chache.

Siyo nyinyi mtu ana pikipiki moja ana wasichana kila mtaa, yeye mwenyewe anataka ale vyakula vizuri avae vizuri na hiyohiyo pikipiki yake moja ajampelekea mwenye pikipiki yake pesa ya siku. Kuweni makini, wekeni bajeti, simamieni malengo yenu hili jina la Dangote halijaja kiurahisi, mkiendelea na imani zenu hizo mtabakia maskini. Pambanane kuliko wengine, muombeni Mungu mtafanikiwa."

Hiyo ilikuwa nukuu kutoka kwa kaka Shabani juu ya utajiri wake. Ndugu zangu vijana kiukweli kaka shabani ni wa kuigwa.
BY: MKAKA WA CHUO.
 
Upvote 2
Kuna mtu Kahama ana bodaboda 300 sijui huyu nae alifreemasika
 
Wapumbavu wanaamini kutajirika ni dawa, Ingekuwa hivyo watz wangekuwa matajiri kweli kweli.
Nani kakuambia utapata utajiri bila jasho.
 
Kaka huyu amanielimisha pakubwa Sana, kwa SABABU amanifanya nitumie Kila chance inayojitokeza katika jamii hata Kama watu wakiidharau, Kama vile bodaboda na uandishi wa Insha na stories Kama hivi pia natumia Kama chance coz NAAMINI siku moja nitafanikiwa
 
Kaka huyu amanielimisha pakubwa Sana, kwa SABABU amanifanya nitumie Kila chance inayojitokeza katika jamii hata Kama watu wakiidharau, Kama vile bodaboda na uandishi wa Insha na stories Kama hivi pia natumia Kama chance coz NAAMINI siku moja nitafanikiwa
Fanya vile vinadharauliwa na Jamii we fanya kisomi.Je wajua ukusanyaji takataka ni utajiri.
 
Kuna mtu Kahama ana bodaboda 300 sijui huyu nae alifreemasika
Ni mtazamo tu lakini Siri ya mafanikio yake analijua yeye mwenyewe. Inaweza kuwa njia sahihi ya upambanaji au njia zisizo za halali, hatuwezi jua pengine alipata Mali za urithi, akauza akanunua hizi pikipiki
 
Back
Top Bottom