"Kaka yake na mke wangu?" Kiswahili gani hicho?

"Kaka yake na mke wangu?" Kiswahili gani hicho?

Joined
Jan 4, 2012
Posts
61
Reaction score
23
Nimekuwa nikiwasikia baadhi ya watu wakiwatambulisha shemeji zao kwamba " huyu ni kaka yake na mke wangu" Kimsingi Kiswahili hicho siyo Sanifu kabisa na wanaokitumia ni bora wakaachana nacho maana ni aibu!

Kiswahili sanifu na fasaha ni; " James ni kaka wa mke wangu! Ukisema James ni kaka yake na mke wangu unazungumzia uwepo wa watu wawili yaani "kaka yake"( kaka wa nani?) na mke wangu. au "His brother" and "my wife"! Kwa mantiki nyingine hapa wanatajwa watu wawili yaani kaka yake mtu fulani na mke wangu> Sentensi hii haioneshi uhusiano wa watu hao wawili bali inataja tu kwamba kuna Kaka yake( mtu fulani) na (mke wangu) mahali hapo! Wala sentensi hiyo haifafanui wanafanya nini mahali hapo! UTATA MTUPU!

Acheni kuharibu Kiswahili!
 
Great teachings mkuu, tupe tiba tupone:rain::rain:
 
Uko sahihi kabisa mkuu. Shida kiswahili cha mitaani kimetawala sana. Na pengine huko shuleni pia walimu hawazungumzi na hawafundishi lugha fasaha ktk ukamilifu wake.
 
Ok..nimeelewa.. "Kaka yake mke wangu" yani mke wangu ni kaka wa mtu fulani..
 
Ok..nimeelewa.. "Kaka yake mke wangu" yani mke wangu ni kaka wa mtu fulani..
 
Back
Top Bottom