Kakae Barack Obama: Kenya Inatawaliwa Na Kabila Moja, Sio Vizuri

Trump2

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
1,553
Reaction score
2,609
Malik Obama, kaka yake Barrack Obama, ameikashifu Kenya kwa anachokiita unafiki - Malik anadai kuwa, Kenya inatawaliwa na kabila moja, Kikuyu - Analinganisha hilo kwa kupewa jina barabara ya Forest jijini Nairobi kuwa Prof. Wangari Maathai - Pia amedai kuwa nyingi ya sekta nchini zina wasimamizi wengi kutoka jamii ya Wakikuyu
Kaka yake aliyekuwa Rais wa Marekani Barrack Obama, Malik Obama, ameichana Kenya na watu wake kwa anachokiita ni unafiki na kutawaliwa na jamii moja. Kwenye ujumbe wake wa Tweeter, Malik anadai kuwa, nchi inatawaliwa na kabila moja na kabila hilo ni jamii ya Wakikuyu.
Ametoa mfano wa barabara ya Forest jijini Nairobi ambayo ilipewa jina la Prof. Wangari Maathai kwa heshima ya Mshindi huyo wa Tuzo la Amani la Nobel mwendazake Wangari Maathai.


Malik Obama (Kulia) anasema Kenya inatawaliwa na kabila moja Picha: BBC

Maathai hadi kifo chake alikuwa mpiganiaji wa uhuru na mtu aliyejali sana hifadhi za mazingira. Kwenye ujumbe wake, Malik anaendelea kusema, sekta zote muhimu Kenya zinaongozwa na watu kutoka kabila la Wakikuyu. Hii ni pamoja na Fedha, kawi, miundombinu na usalama. Madai yake yanajiri huku joto la kisiasa nchini likiendelea kuwa lisiloelezeaka kufuatia chaguzi za Agosti 8 na Oktoba 26.

Malik ameichana Kenya kwa kuwa taifa lenye unafiki mkubwa Picha: BBC

Rais Uhuru Kenyatta alichaguliwa na kuapishwa huku Upinzani National Super Alliance (NASA) ukilalamika na kutangaza kutomtambua Rais. Kinara Mkuu wa NASA Raila Odinga ametaja kuwa, ataapishwa Desemba 12, 2017, wiki tatu baada ya Uhuru kuapishwa

Kenya inatawaliwa na kabila moja tu na sio vizuri, asema kakake Barack Obama | TANZANIA CLASSIC
 
Hv kudadadek Sasa wote nyie si wafrika mambo ya ukabila ni ujinga sana
 
Ukabila utaendelea kulitafuna taifa hilo ingawa cha kushangaza wakenya wenyewe wanaonyesha kuifurahia hali hiyo!!! Nashukuru Mungu kunifanya kuwa Mtanzania
Kuna faraja gani kuwa Mtanzania? Watu wanauawa, maisha magumu, nchi iko nyuma kimaendeleo ukilinganisha na kenya. Hakuna cha kujivunia kama kweli unafatilia ukweli wa mambo kwa nchi hii.
 
Kuna faraja gani kuwa Mtanzania? Watu wanauawa, maisha magumu, nchi iko nyuma kimaendeleo ukilinganisha na kenya. Hakuna cha kujivunia kama kweli unafatilia ukweli wa mambo kwa nchi hii.
Kenya wanaweza kujivunia maendeleo gani kwenye taifa ambalo kama wewe si mkikuyu huna chako? Ni heri nibakie kuwa mbwa masikini na huru wa manzese kuliko kujivunia kuwa mbwa uliyefungwa minyororo huko masaki.
 
Kenya wanaeweza kujivunia maendeleo gani kwenye taifa ambalo kama wewe si mkikuyu huna chako? Ni heri nibakie kuwa mbwa masikini na huru wa manzese kuliko kujivunia kuwa mbwa uliyefungwa minyororo huko masaki.
Tanzania kama siyo CCM unaweza kujivunia? Ni bora ukikuyu kuliko U-CCM; Sina cha kujivunia na taifa hili, heri kuishi Somalia kuliko Tanzania ambako serikali inapiga risasi watu mchana kweupe.
 
Magufuli nae anaendekeza wasukumba na Lake zone mwache hiyo mbegu anayoipanda inaota.
 
Ukabila utaendelea kulitafuna taifa hilo ingawa cha kushangaza wakenya wenyewe wanaonyesha kuifurahia hali hiyo!!! Nashukuru Mungu kunifanya kuwa Mtanzania
Hata Tanzania kuna tatizo. Ila haturuhusiwbai kujadili:+
Mfano upande wa kisiasa:-
Tunatawaliwa na chama kimoja, demokrasia yetu imejaa unafiki sana.

Pia ukabila umeota mabawa sana zamu hii;-

Maeneo ambago CCM, imepoteza kwenye Uchaguzi 2015, yamekua yakibaguliwa kupata huduma za kimaendeleo sana tu.

Kwahiyo kila taifa lina unafiki wake. Tupambane na hali zetu kwanza. tung'oe boriti zetu kabla hatujatazama kibanzi kwa jicho la majirani zetu wakenya.

All in all tawala zote duniani ni lazima kua kuna tabaka ambalo linashika hatamu za uongozi kwa nchi yoyote. Hata iwe USA.
 
Mada iliyopo mbele yetu ni ukabila kwenye siasa. Kati ya maraisi wanne waiotawala taifa hilo watatu wanatoka kabila lile lile. Suala la kubaguliwa kwa kuwa hamkuichagua CCM ni mada nyingine. Vinginevyo ukabila wa Kenya mbali ya kisiasa, umetamalaki kwenye maeneo mengine ya kijamii. Tofauti sana tunavyoishi na kuendesha mambo yetu Tanazania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…