Kakobe amponza muumini wizarani

1. Kakobe is wrong for not giving Caesar his.
2. His followers are naive for being misled.
3. The Ministry is wrong for being ambiguous.
 
Ni rahisi sana kwa Bosi kumuhamisha/kuhama na katibu muhtasi............not to disrespect the katibu muhtasis.........lakini ndio ukweli wenyewe.........huyo Mtweve ni kutokana na mazingira yaliyopo amejichangia kujihamisha (mavazi)..............hata ningekuwa mimi ndio Bosi wake ningekosa imani na yeye.....na kuomba HR waniletee mwingine..............na ndilo jambo lililofanyika.............huyo kamishna wa Kanda ya Mashariki naye kakosa ya kuongea mpaka amuulize Mtweve swali lile?..........Stupid kamishna!
 
Madai kama haya bila uthibitisho inaweza kulipelekea taifa kwenye kulipa fidia zisizo na kichwa wala miguu. Wizara imethibitisha kama huyu mfanyakazi ndiye aliyefanya hilo? Hivi hizi wizara zina wanasheria kweli? Kama huyu mama hajafanya hayo wanayomtuhumu na akiwaburuta mahakamani itakuwa ni kumlipa fidia.

Kuna watumishi wengi wanafanyiwa mambo kama haya na serikali,mwisho serikali inaishia kulipa kwa maamuzi ya vichaa kama hawa. Kama ni kweli alivujisha siri za ofisi anatakiwa asimamishwe au ahamishwe,lakini baada ya ushahidi kupatikana siyo kwa hisia tu, au kwa sababu anasali pale, au kwa sababu huwa anavaa tshirt za kupinga umeme kupita pale.

Kila mtu ana haki ili mradi havunji sheri ya nchi. Kupinga umeme kupita aple hakuna uvunjaji wa sheria yoyote,ila TANESCO kupitisha umeme pale ni kuvunja sheria kwani ni karibu na makazi ya watu. Inatakiwa watu waondolewe ndipo umeme upite au umeme upite mahali pengine.
 

swali chafu??
 
Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni (Farao)!!! Maswala ya imani ya mtu ni conflict of interest au?? Kama dada alipeleka barua kama sehemu ya kazi yake ya kusambaza barua maeneo mengine kama ilivyokuwa kwa Kakobe kuna tatizo gani? Kweli inashangaza!!
 
Unajua sometimes kuna Mambo ya Ajabu sana Iweje uvae tisheti ya Kuilaani Ofisi yako? Huyo dada naye alizidisha sana Ushabiki LoL! Ni Sawa na Mfanyakazi wa Wizara ya Mambo ya ndani anatinga Kazini na Fulana iliyoandikwa "Jeshi la Polisi Limeoza" Unategemea nini kama si kuwatafutia watu Sababu
 
Jamani acheni jazba,

Hapa katibu muhtasi amehamishwa idara ndani ya wizara husika. Sidhani kama kuhamishwa idara ni sawa na kuwa demoted. Katibu Muhtasi (Secretary) kupelekwa kwa bosi mwingine sidhani kama ni tatizo. Ila inawezekana kwa njia moja au nyingine ni kweli alikuwa akifujisha siri kwani yeye mafaili yote lazima yapite kwake.
 
Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, David Ngairo, kuzungumzia suala hilo, alishindwa kukubali wala kukanusha na badala yake kumtaka mwandishi wa habari hizi kumweleza ni wapi alikozipata taarifa hizo.

David Ngairo ni nani???
 
Wapi tatizo?mawaziri,wakurugenzi na hata muajiriwa yeyote anatakiwa kwenda kufanya mahali popote atakapo pangiwa na muajiri wake,jamani acheni kuingiza mambo ya kakobe kwenye masuala ya kazi.
 
Umafia unaingizwa nchini?

Well sijafuatialia sakata la huu umeme toka mwanzo lakini naomba msaada wa kufafanuliwa yafuatayo

1. Ni lazima umeme upite hapo?
2. Hakuna uwezekano wa kuongezea line kwenye njia zilizopo kitaalam; na kama hii ni kweli vipi mahitaji ya kikua tuseme in 15 yrs to come wanaweka nguzo nyingine tena sehemu nyingine; in 50 yr tutakuwa na line za high volatage ngapi?

Nawaza kwa sauti!
 
Hivi ujinga huu utaisha lini?Kwa hiyo ile haki ya kuabudu haipo tena?Je,wanajua ni wafanyakazi wangapi wa wizara husika wanaoabudu kwa bwana Zacharia(Kakobe)?Aaaaaghhhhhhhhhhh!!
 
Hats Jesus alisema, huwezi kutumikia mabwana wawili, kama alikuwa anahujumu kwa kutoa siri za wizara na kupeleka kwa mtaalamu Kakobe, hafai kubaki hapo wizarani. Brainwashed, kama wengine wanaopeleka mafao kwa mtaalmu Kakobe...
 
Hivi ujinga huu utaisha lini?Kwa hiyo ile haki ya kuabudu haipo tena?Je,wanajua ni wafanyakazi wangapi wa wizara husika wanaoabudu kwa bwana Zacharia(Kakobe)?Aaaaaghhhhhhhhhhh!!

Hakuna mwajiri atakayekubali kukaa na mfanyakazi anayevujisha siri au nyaraka muhimu za muajiri yake. dada devotha alikuwa na mapungufu ya kimaadili na hii inawezekana na baadhi ya imani potofu wanazopata huko wanakoabudu
 
Kama iligundulika yeye ni muumini wa Kakobe na huwa anavaa zile tshirt za njano na siri zimevuja basi anastahili kuhamishwa hata kufukuzwa ikibidi maana siku hizi wafanayakazi wamekosa uadilifu kabisa.....ndio maana kakobe ana kiburi kumbe huwa anamegewa taarifa
 
Hats Jesus alisema, huwezi kutumikia mabwana wawili, kama alikuwa anahujumu kwa kutoa siri za wizara na kupeleka kwa mtaalamu Kakobe, hafai kubaki hapo wizarani. Brainwashed, kama wengine wanaopeleka mafao kwa mtaalmu Kakobe...


Sosoliso mbona tayari unamhukumu dada Dorothy? Unao ushahidi kuwa amevujisha hizo unazozisema ni siri?

Na kama amevujisha basi hafai hata kubaki kazini; iweje adhabu yake iwe ni kumhamisha?

Mwisho Kakobe ni askofu; basi walau mwite Kakobe tu usimdhihaki kwa kumwita Mtaalamu.
 

Well said mkuu!! Hata mimi ningekuwa bosi wake ningemfukuza kazi!! Naona kama kaonewa huruma, pengine wamemuonea huruma kakobe kwamba hatakosa fungu la kumi toka kwa muumini wake huyo!!

Kwa uzoefu nilionao, waumini wa Kakobe ni kama mazezeta (samahani kama nitamkwaza mtu kwa kutumia neno hilo). Kwa wao kukesha pale ati kuwazuia Tanesco kupitisha nyaya za umeme, ni wazi waumini wa Kakobe hawana uwezo wa kuchambua mambo hata ya 1+1. Binafsi naona Kakobe alitakiwa aende mahakamani kusimamisha ujenzi wa hiyo minara, na sio kutumia nguvu kuwazuia tanesco.

Kwa hiyo kama waumini wote wanaweza kukubaliana na maamuzi ya askofu wao kukesha pale, je atashindweje huyo dada kumvujishia siri za wizara askofu kakobe???

Pili huyo dada anadiriki kuvaa tisheti inayoiashifu wizara anayoifanyia kazi, huu ni upuuzi kabisa. Hii yote inaonyesha jinsi gani haya makanisa yanavyotumia vibaya na hawa wanaojiita wachungaji/manabii/maaskofu/mitume/wazee wa upako n.k n.k!

Ni wakati wa serikali kuanzisha regulatory agency ya kusimamia mienendo ya hizi taasisi za dini, vinginevyo tutashuhudia mambo mengi ya ajabu hapa nchini!
Huyo dada asitake kujitetea
 

Kuna taratibu za kumfukuza mtu kazi akiwa serikalini..hilo linaweza kuwa kama onyo tu....afu huyu kakobe huo U-Askofu alijipa mwenyewe au wafadhili wake wa marekani ndo walimtunuku title hiyo??
Binafsi mda mrefu sana sina IMANI nae huyu ndugu Kakobe sijui anawaahada vp waumini na wengi wao ni wakina mama
 
Pole yake ,ajifunze kutenganisha kanisa na kazi.Ya Kaisari apewe Kaisari na ya MUNGU apewe MUNGU>
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…