kioju
JF-Expert Member
- Apr 28, 2014
- 804
- 271
 12:41
Akihubiri siku ya Pasaka
katika Kanisa la Full Gospel
Bible Fellowship lililopo
Mwenge katika Jiji la Dar-Es-
Salaam, Askofu Mkuu Zachary
Kakobe alisema kwamba,
inajulikana wazi kwamba
Lowassa amekuwa anautaka
Urais kwa udi na uvumba
kwa miaka mingi, hata
mwaka 1995 alijitosa
hadharani kuuwania, sasa
anapodai kwamba hivi sasa
kuna makundi
yanayokwenda kwake
kumshawishi agombee Urais,
kana kwamba yeye hataki
Urais, anakuwa
anamdanganya nani?
Ingawa katika mahubiri hayo
ya saa mbili, Kakobe
hakumtaja Lowassa kwa jina,
hata hivyo Kakobe alisema,
"Wako watu wengine ambao
inajulikana wazi kwamba
wamekuwa wakiutaka Urais
kwa udi na uvumba, kwa
miaka mingi, lakini hivi sasa
wanasema kuna makundi ya
watu yanawafuata nyumbani,
kuwashawishi kugombea
Urais; kama vile hawautaki
Urais, hivi watu hawa
wanamdanganya nani?
"Na wale wanaokwenda
kumshawishi mtu ambaye
kwa miaka mingi,
anajulikana kwamba
anautaka Urais, hawajui
kwamba nao wanafanywa
kuwa wajinga? Mtu
anayejulikana kwa muda
mrefu kwamba anautaka
Urais, ni vema akatangaza tu
moja kwa moja nia yake, bila
haja ya ghiliba."
Katika mahubiri yake yenye
kichwa, "UPOTOSHAJI WA
UKWELI", Kakobe alieleza
jinsi Gavana wa Kirumi, au
liwali Pontio Pilato,
alivyojiunga na Viongozi
wengine kupotosha ukweli wa
kufufuka kwa Yesu, na
kusema kwamba wanafunzi
wake waliuiba mwili wake,
wakati askari walinzi
walipokuwa wamelala, na
kuwadanganya watu, ingawa
wao wenyewe waliujua
ukweli.
"Pilato aliwadanganya watu
hao kwa muda tu, lakini
hatimaye ukweli ulikuwa
dhahiri, walipomwona Yesu
kati yao kwa muda wa siku
40. Unaweza kuwadanganya
watu kwa muda tu, lakini
hatimaye ukweli hudhihirika,
na kumfedhehesha yule
aliyeupotosha ukweli huo",
alisema.
Aliendelea kusema kuwa, hata
leo kuna upotoshaji wa kweli
mbalimbali za kiroho na
kimwili. Baada ya kuelezea
juu ya baadhi ya kweli za
kiroho zilizopotoshwa,
aliwageukia wanasiasa
waongo, akianza kwa kutoa
mfano wa Waziri wa Habari
wa Iraq, wakati wa vita ya
mwaka 2003, Muhammad
Saeed al-Sahhaf, aliyekuwa
akipotosha ukweli kuhusu
jinsi Iraq ilivyokuwa
inapigwa vibaya katika vita
hivyo, na akaendelea kusema;
"Kabla sijaendelea, nifafanue
kwanza juu ya watu
wanaopotosha ukweli, kwa
kusema kwamba eti
Wachungaji hawapaswi
kuwakemea wanasiasa
wananapopotoka. Watu hawa
hawajui Biblia. Katika
MAMBO YA WALAWI
4:22-23, Biblia inasema,
Mtawala akifanya dhambi,
inampasa Kuhani yaani
Mchungaji, kumjulisha
dhambi yake."
Kakobe aliendelea kusema
kwamba huu ni mwaka wa
Uchaguzi, hivyo Watanzania
wawe makini na wanasiasa
waongo wanaofanya uongo
kuwa sehemu ya siasa zao.
"Siasa, ni Sayansi, inaitwa
POLITICAL SCIENCE, na "any
kind of science only deals
with facts". Wanasiasa
hawana budi kuwa wakweli
kwa kuwa siasa ni sayansi.
"Siasa siyo mchezo mchafu,
bali baadhi ya wanasiasa
ndiyo wachafu.
Msidanganywe tena na
wanasiasa ambao watakuja
kwenu mwaka huu na ahadi
za uongo za kuibadili miji na
kuifanya kuwa kama New
York, kwa miaka mitano; na
wengine hawana AIBU,
wanaweza hata kuwaambia
wakazi wa Dodoma kwamba
watawaletea meli! Hamna
budi kuyachunguza kwa
makini maneno yao, na
kuona kama ni ya kweli."
Kuhusu Katiba, Kakobe
aliwaunga mkono Maaskofu
waliowapa Wakristo
maelekezo ya kuikataa Katiba
Pendekezwa, katika Kura ya
Maoni, na kusema kwamba
hiyo ndiyo kazi ya Mchungaji.
"Mchungaji, pia ni Mwalimu,
kazi yake ni kuchunga na pia
kulisha kondoo (YOHANA
21:15-17), na Biblia
inafafanua juu ya kazi ya
Mwalimu katika ISAYA
30:20-21, ikieleza kwamba
Mwalimu anatakiwa
kuwaambia anaowaongoza,
"Njia ni hii ifuateni,
wageukapo kwenda kulia au
kushoto".
Aliendelea kusema,
"Kumekuwa na udanganyifu
au upotoshaji wa ukweli
kuhusu Katiba, tangu katika
hatua za mwanzo kabisa za
mchakato wa Katiba, ambapo
Chama kimoja cha siasa,
kiliwapachika makada wake
katika vikundi mbalimbali, ili
kiwe na wajumbe wengi.
"Kwa mfano Kingunge
Ngombale Mwiru
aliwawakilisha waganga wa
kienyeji, lakini cha ajabu,
ukienda kwake hata leo,
hakuna kibao kwake
kinachozitambulisha kazi
zake za uganga wa kienyeji,
kama ilivyo kwa waganga
wengine! Siyo hilo tu, kote
duniani, Katiba yoyote ya
nchi, lazima itokane na
muafaka wa Kitaifa, ili Katiba
hiyo iwe na sifa ya kusomeka
katika Utangulizi wake, "SISI
WANANCHI".
"Hapa kwetu, watawala
hawakutaka kabisa muafaka
katika kutengeneza Katiba
yetu, lakini wanadai eti,
Katiba Pendekezwa, ni bora
kuliko zote Afrika! Huu ni
upotoshaji wa ukweli, wa hali
ya juu sana."
Aliendelea kusema kwamba,
Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba na Sheria ya Kura ya
Maoni, hazikuzingatiwa
kikamilifu katika mchakato
huo uliojaa udanganyifu.
"Sheria ya Kura ya Maoni,
Ibara ya 5(3), inasema
kwamba kungetakiwa
kuwepo na elimu kwa wapiga
kura, kwa siku 60, mara tu
baada ya Tangazo la Katiba
Pendekezwa katika Gazeti la
Serikali Na. 382 lililotolewa
tarehe 10.10.2014, lakini
elimu hiyo iliyopaswa
kutolewa na Tume ya
Uchaguzi, haijafanyika hadi
hivi leo!
V"ilevile, Sheria ya Kura ya
Maoni Ibara ya 4(3) na 4(4),
inasema kwamba
kungetakiwa kutangazwa
katika Gazeti la Serikali,
SWALI LA KURA YA MAONI,
ambalo wananchi wangelijibu
kwa jibu la NDIYO au
HAPANA, na pia Sheria ya
Kura ya Maoni Ibara ya 12(1)
na 12(2) na Ibara ya 16(1)
inasema kwamba,
kungetakiwa kuwepo na
Kamati mbili za Kura ya
Maoni, Kamati moja ya
NDIYO, na nyingine ya
HAPANA, ambazo
zingejumuisha wananchi
wenye misimamo tofauti
kutoka katika makundi
mbalimbali katika jamii, na
Kamati hizo zingepiga
kampeni kwa siku 30.
"Yote haya hayakuzingatiwa,
lakini kinyume chake,
Watawala hadi hivi leo,
hawataki hata kusikia watu
wakisema HAPANA kwa Kura
ya Maoni, na wakati huohuo,
wengine bado wanataka Kura
ya Maoni ifanyike Aprili 30,
pamoja na kwamba
imetangazwa na Tume ya
Uchaguzi, kwamba
imeahirishwa!
"Wachungaji wengine wenye
njaa, wanathubutu kusema
kwamba eti kwa sababu
kwenye Katiba Pendekezwa
kuna Uhuru wa kuabudu, basi
sisi Wachungaji tukae kimya,
mengine hayatuhusu, hawa
wana njaa kali, na upeo
mdogo wa uelewa wa mambo
haya.
"Mimi sina njaa, na ninasema
kwa msisitizo, Katiba ni zaidi
ya Uhuru wa kuabudu.
Ilikuwa rahisi kwa Pilato
kuwadanganya watu wa
nyakati hizo, lakini leo ni
kazi sana kuwadanganya
watu wanaopata maarifa na
habari juu ya yote
yanayofanyika kote duniani,
kwa TV, Redio, Magazeti,
Intaneti na Mitandao ya
kijamii.
"Watu wanajua kwamba kote
ulimwenguni, Katiba ya
Wananchi hutokana na
muafaka, na Kura ya Maoni,
hufanyika baada ya Kampeni
ya NDIYO na HAPANA, kama
ilivyofanyika Kenya ambako
waliosema NDIYO waliitwa
kundi la NDIZI, na waliosema
HAPANA waliitwa kundi la
CHUNGWA.
"Waliowaambia Wakristo
wapige kura ya HAPANA
kwenye Kura ya Maoni,
ninawapa asilimia 90, hata
hivyo kwa unyenyekevu,
mimi ninaomba kuhitilafiana
nao, kwa kuongeza kwamba
Kura ya Maoni inapaswa
kususiwa kabisa, kwa sababu
kushiriki katika Kura hiyo, ni
kuuhalalisha udanganyifu wa
Watawala hawa, na
kujifedhehesha mwishoni.
"Tangu mwanzo, watu hawa
walitumia ubabe na wizi wa
kura wa dhahiri katika Bunge
la Katiba, na kutangaza kura
feki za NDIYO za mahujaji na
wajumbe wengine ambao
hawakuwepo ukumbini
wakati wa kupiga kura, na
pia kura za Wazanzibari feki,
na hivyo kupitisha kwa
lazima, Katiba Pendekezwa.
"Wamedhamiria kufanya
hivyohivyo hata katika Kura
ya Maoni, ili kuipitisha kwa
lazima Katiba yao
Pendekezwa; ukizingatia
kwamba, ili kutimiza kusudi
hilo, wameweka sheria
mbaya kwa makusudi ya
kuhalalisha udanganyifu.
"Kwa mfano Sheria ya Kura
ya Maoni Ibara ya 34(2),
inahalalisha wapiga kura
walioandikishwa Tanzania
Bara, kwenda kupiga kupiga
Kura ya Maoni, huko
Zanzibar. Katika mazingira
haya, Kura za HAPANA
zitasaidia nini? Ni
kuhalalisha tu udanganyifu
wao, na kujifedhehesha.
"Mwandishi Mkuu wa Katiba
Pendekezwa, yeye mwenyewe
amesema anapenda aitwe
JOKA LA MAKENGEZA!
Niliposikia juu ya Jina lake
hili, nilipigwa na butwaa!
Katika Biblia, Joka ni Ibilisi
au Shetani (UFUNUO 12:7-9;
20:1-2), maana yake ni
kwamba Mwandishi Mkuu wa
Katiba Pendekezwa, ni Joka
yaani Shetani, na hivyo
tunaweza kusema Katiba hiyo
ni ya Kishetani, maana
imetokana na Shetani
ambaye ni Joka lililoko
kuzimu!
"Kumbe basi, siyo tu kwamba
Katiba Pendekezwa
imeahirishwa, ila ni kwamba
Mungu ameikataa tangu siku
ya kwanza ya mchakato
wake!
"Kwa sasa tuwaze tu
kujiandikisha kwa wingi
katika Uandikishaji wa
Wapiga Kura, kwa BVR, na
kuwa tayari tu kwa Uchaguzi
Mkuu, na kuisahau kabisa
Kura ya Maoni."
Akihubiri siku ya Pasaka
katika Kanisa la Full Gospel
Bible Fellowship lililopo
Mwenge katika Jiji la Dar-Es-
Salaam, Askofu Mkuu Zachary
Kakobe alisema kwamba,
inajulikana wazi kwamba
Lowassa amekuwa anautaka
Urais kwa udi na uvumba
kwa miaka mingi, hata
mwaka 1995 alijitosa
hadharani kuuwania, sasa
anapodai kwamba hivi sasa
kuna makundi
yanayokwenda kwake
kumshawishi agombee Urais,
kana kwamba yeye hataki
Urais, anakuwa
anamdanganya nani?
Ingawa katika mahubiri hayo
ya saa mbili, Kakobe
hakumtaja Lowassa kwa jina,
hata hivyo Kakobe alisema,
"Wako watu wengine ambao
inajulikana wazi kwamba
wamekuwa wakiutaka Urais
kwa udi na uvumba, kwa
miaka mingi, lakini hivi sasa
wanasema kuna makundi ya
watu yanawafuata nyumbani,
kuwashawishi kugombea
Urais; kama vile hawautaki
Urais, hivi watu hawa
wanamdanganya nani?
"Na wale wanaokwenda
kumshawishi mtu ambaye
kwa miaka mingi,
anajulikana kwamba
anautaka Urais, hawajui
kwamba nao wanafanywa
kuwa wajinga? Mtu
anayejulikana kwa muda
mrefu kwamba anautaka
Urais, ni vema akatangaza tu
moja kwa moja nia yake, bila
haja ya ghiliba."
Katika mahubiri yake yenye
kichwa, "UPOTOSHAJI WA
UKWELI", Kakobe alieleza
jinsi Gavana wa Kirumi, au
liwali Pontio Pilato,
alivyojiunga na Viongozi
wengine kupotosha ukweli wa
kufufuka kwa Yesu, na
kusema kwamba wanafunzi
wake waliuiba mwili wake,
wakati askari walinzi
walipokuwa wamelala, na
kuwadanganya watu, ingawa
wao wenyewe waliujua
ukweli.
"Pilato aliwadanganya watu
hao kwa muda tu, lakini
hatimaye ukweli ulikuwa
dhahiri, walipomwona Yesu
kati yao kwa muda wa siku
40. Unaweza kuwadanganya
watu kwa muda tu, lakini
hatimaye ukweli hudhihirika,
na kumfedhehesha yule
aliyeupotosha ukweli huo",
alisema.
Aliendelea kusema kuwa, hata
leo kuna upotoshaji wa kweli
mbalimbali za kiroho na
kimwili. Baada ya kuelezea
juu ya baadhi ya kweli za
kiroho zilizopotoshwa,
aliwageukia wanasiasa
waongo, akianza kwa kutoa
mfano wa Waziri wa Habari
wa Iraq, wakati wa vita ya
mwaka 2003, Muhammad
Saeed al-Sahhaf, aliyekuwa
akipotosha ukweli kuhusu
jinsi Iraq ilivyokuwa
inapigwa vibaya katika vita
hivyo, na akaendelea kusema;
"Kabla sijaendelea, nifafanue
kwanza juu ya watu
wanaopotosha ukweli, kwa
kusema kwamba eti
Wachungaji hawapaswi
kuwakemea wanasiasa
wananapopotoka. Watu hawa
hawajui Biblia. Katika
MAMBO YA WALAWI
4:22-23, Biblia inasema,
Mtawala akifanya dhambi,
inampasa Kuhani yaani
Mchungaji, kumjulisha
dhambi yake."
Kakobe aliendelea kusema
kwamba huu ni mwaka wa
Uchaguzi, hivyo Watanzania
wawe makini na wanasiasa
waongo wanaofanya uongo
kuwa sehemu ya siasa zao.
"Siasa, ni Sayansi, inaitwa
POLITICAL SCIENCE, na "any
kind of science only deals
with facts". Wanasiasa
hawana budi kuwa wakweli
kwa kuwa siasa ni sayansi.
"Siasa siyo mchezo mchafu,
bali baadhi ya wanasiasa
ndiyo wachafu.
Msidanganywe tena na
wanasiasa ambao watakuja
kwenu mwaka huu na ahadi
za uongo za kuibadili miji na
kuifanya kuwa kama New
York, kwa miaka mitano; na
wengine hawana AIBU,
wanaweza hata kuwaambia
wakazi wa Dodoma kwamba
watawaletea meli! Hamna
budi kuyachunguza kwa
makini maneno yao, na
kuona kama ni ya kweli."
Kuhusu Katiba, Kakobe
aliwaunga mkono Maaskofu
waliowapa Wakristo
maelekezo ya kuikataa Katiba
Pendekezwa, katika Kura ya
Maoni, na kusema kwamba
hiyo ndiyo kazi ya Mchungaji.
"Mchungaji, pia ni Mwalimu,
kazi yake ni kuchunga na pia
kulisha kondoo (YOHANA
21:15-17), na Biblia
inafafanua juu ya kazi ya
Mwalimu katika ISAYA
30:20-21, ikieleza kwamba
Mwalimu anatakiwa
kuwaambia anaowaongoza,
"Njia ni hii ifuateni,
wageukapo kwenda kulia au
kushoto".
Aliendelea kusema,
"Kumekuwa na udanganyifu
au upotoshaji wa ukweli
kuhusu Katiba, tangu katika
hatua za mwanzo kabisa za
mchakato wa Katiba, ambapo
Chama kimoja cha siasa,
kiliwapachika makada wake
katika vikundi mbalimbali, ili
kiwe na wajumbe wengi.
"Kwa mfano Kingunge
Ngombale Mwiru
aliwawakilisha waganga wa
kienyeji, lakini cha ajabu,
ukienda kwake hata leo,
hakuna kibao kwake
kinachozitambulisha kazi
zake za uganga wa kienyeji,
kama ilivyo kwa waganga
wengine! Siyo hilo tu, kote
duniani, Katiba yoyote ya
nchi, lazima itokane na
muafaka wa Kitaifa, ili Katiba
hiyo iwe na sifa ya kusomeka
katika Utangulizi wake, "SISI
WANANCHI".
"Hapa kwetu, watawala
hawakutaka kabisa muafaka
katika kutengeneza Katiba
yetu, lakini wanadai eti,
Katiba Pendekezwa, ni bora
kuliko zote Afrika! Huu ni
upotoshaji wa ukweli, wa hali
ya juu sana."
Aliendelea kusema kwamba,
Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba na Sheria ya Kura ya
Maoni, hazikuzingatiwa
kikamilifu katika mchakato
huo uliojaa udanganyifu.
"Sheria ya Kura ya Maoni,
Ibara ya 5(3), inasema
kwamba kungetakiwa
kuwepo na elimu kwa wapiga
kura, kwa siku 60, mara tu
baada ya Tangazo la Katiba
Pendekezwa katika Gazeti la
Serikali Na. 382 lililotolewa
tarehe 10.10.2014, lakini
elimu hiyo iliyopaswa
kutolewa na Tume ya
Uchaguzi, haijafanyika hadi
hivi leo!
V"ilevile, Sheria ya Kura ya
Maoni Ibara ya 4(3) na 4(4),
inasema kwamba
kungetakiwa kutangazwa
katika Gazeti la Serikali,
SWALI LA KURA YA MAONI,
ambalo wananchi wangelijibu
kwa jibu la NDIYO au
HAPANA, na pia Sheria ya
Kura ya Maoni Ibara ya 12(1)
na 12(2) na Ibara ya 16(1)
inasema kwamba,
kungetakiwa kuwepo na
Kamati mbili za Kura ya
Maoni, Kamati moja ya
NDIYO, na nyingine ya
HAPANA, ambazo
zingejumuisha wananchi
wenye misimamo tofauti
kutoka katika makundi
mbalimbali katika jamii, na
Kamati hizo zingepiga
kampeni kwa siku 30.
"Yote haya hayakuzingatiwa,
lakini kinyume chake,
Watawala hadi hivi leo,
hawataki hata kusikia watu
wakisema HAPANA kwa Kura
ya Maoni, na wakati huohuo,
wengine bado wanataka Kura
ya Maoni ifanyike Aprili 30,
pamoja na kwamba
imetangazwa na Tume ya
Uchaguzi, kwamba
imeahirishwa!
"Wachungaji wengine wenye
njaa, wanathubutu kusema
kwamba eti kwa sababu
kwenye Katiba Pendekezwa
kuna Uhuru wa kuabudu, basi
sisi Wachungaji tukae kimya,
mengine hayatuhusu, hawa
wana njaa kali, na upeo
mdogo wa uelewa wa mambo
haya.
"Mimi sina njaa, na ninasema
kwa msisitizo, Katiba ni zaidi
ya Uhuru wa kuabudu.
Ilikuwa rahisi kwa Pilato
kuwadanganya watu wa
nyakati hizo, lakini leo ni
kazi sana kuwadanganya
watu wanaopata maarifa na
habari juu ya yote
yanayofanyika kote duniani,
kwa TV, Redio, Magazeti,
Intaneti na Mitandao ya
kijamii.
"Watu wanajua kwamba kote
ulimwenguni, Katiba ya
Wananchi hutokana na
muafaka, na Kura ya Maoni,
hufanyika baada ya Kampeni
ya NDIYO na HAPANA, kama
ilivyofanyika Kenya ambako
waliosema NDIYO waliitwa
kundi la NDIZI, na waliosema
HAPANA waliitwa kundi la
CHUNGWA.
"Waliowaambia Wakristo
wapige kura ya HAPANA
kwenye Kura ya Maoni,
ninawapa asilimia 90, hata
hivyo kwa unyenyekevu,
mimi ninaomba kuhitilafiana
nao, kwa kuongeza kwamba
Kura ya Maoni inapaswa
kususiwa kabisa, kwa sababu
kushiriki katika Kura hiyo, ni
kuuhalalisha udanganyifu wa
Watawala hawa, na
kujifedhehesha mwishoni.
"Tangu mwanzo, watu hawa
walitumia ubabe na wizi wa
kura wa dhahiri katika Bunge
la Katiba, na kutangaza kura
feki za NDIYO za mahujaji na
wajumbe wengine ambao
hawakuwepo ukumbini
wakati wa kupiga kura, na
pia kura za Wazanzibari feki,
na hivyo kupitisha kwa
lazima, Katiba Pendekezwa.
"Wamedhamiria kufanya
hivyohivyo hata katika Kura
ya Maoni, ili kuipitisha kwa
lazima Katiba yao
Pendekezwa; ukizingatia
kwamba, ili kutimiza kusudi
hilo, wameweka sheria
mbaya kwa makusudi ya
kuhalalisha udanganyifu.
"Kwa mfano Sheria ya Kura
ya Maoni Ibara ya 34(2),
inahalalisha wapiga kura
walioandikishwa Tanzania
Bara, kwenda kupiga kupiga
Kura ya Maoni, huko
Zanzibar. Katika mazingira
haya, Kura za HAPANA
zitasaidia nini? Ni
kuhalalisha tu udanganyifu
wao, na kujifedhehesha.
"Mwandishi Mkuu wa Katiba
Pendekezwa, yeye mwenyewe
amesema anapenda aitwe
JOKA LA MAKENGEZA!
Niliposikia juu ya Jina lake
hili, nilipigwa na butwaa!
Katika Biblia, Joka ni Ibilisi
au Shetani (UFUNUO 12:7-9;
20:1-2), maana yake ni
kwamba Mwandishi Mkuu wa
Katiba Pendekezwa, ni Joka
yaani Shetani, na hivyo
tunaweza kusema Katiba hiyo
ni ya Kishetani, maana
imetokana na Shetani
ambaye ni Joka lililoko
kuzimu!
"Kumbe basi, siyo tu kwamba
Katiba Pendekezwa
imeahirishwa, ila ni kwamba
Mungu ameikataa tangu siku
ya kwanza ya mchakato
wake!
"Kwa sasa tuwaze tu
kujiandikisha kwa wingi
katika Uandikishaji wa
Wapiga Kura, kwa BVR, na
kuwa tayari tu kwa Uchaguzi
Mkuu, na kuisahau kabisa
Kura ya Maoni."