Kakobe: Ninaunga mkono Ukawa kususia Bunge

Kakobe: Ninaunga mkono Ukawa kususia Bunge

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
3,098
Reaction score
631
Dar es Salaam. Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe ameongeza chumvi katika Mchakato wa Katiba kwa kueleza kuwa anaunga mkono msimamo wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutorejea kwenye awamu ya pili ya vikao vya Bunge Maalumu la Katiba.

Kakobe pia alimtupia lawama Rais Jakaya Kikwete akisema hotuba yake ya kufungua Bunge hilo ndiyo chanzo cha kuvuruga mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya.

Kakobe ametoa kauli hiyo zikiwa zimepita takriban siku tatu tangu Rais Kikwete alipotoa hotuba yake ya kila mwezi na kujivua lawama hizo alizokuwa akitupiwa na watu wa kada mbalimbali.

“Naunga mkono Ukawa si kwa asilimia 100 bali asilimia 150 kwa msimamo wao wa kususia vikao. Tena sitegemei kusikia wamerejea bungeni, wakirejea watakuwa wamelogwa. Lazima wahakikishe upungufu huo unafanyiwa kazi kabla ya kurejea kwenye awamu ya pili ya vikao hivyo vilivyopangwa kuanza Agosti 5,” alisema.

Aliongeza: “Pengine kilichoonekana kuwa kibaya ni jinsi nilivyozifasiri taarifa hizo na mapendekezo ya Tume. Sioni kosa langu ni kutoa maoni kuhusu baadhi ya vipengele vya rasimu kwa sababu imetolewa hadharani kwa watu kuijadili. Mimi kama raia ninayo haki ya kufanya hivyo kama wafanyavyo wengine,” alisema Kikwete kwenye hotuba hiyo.

Hata hivyo, jana Kakobe aliyezungumza kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Kanisa la FGBF alisema kuwa anapingana na utetezi huo kwani hauna hoja ya msingi kwani alishavuruga mchakato huo tangu awali.

“Hotuba yake ya kufungua Bunge hilo ndiyo iliyoharibu mambo yote hadi sasa tumefika katika hali hii.Anafanya hivyo akiwa na dhamira ya kuvuruga mchakato huo ili usiendelee kwa kuhofia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuanguka katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Mapendekezo ya wananchi, ambayo yameorodheshwa kwenye rasimu, yanakinzana na matakwa ya chama hicho hiyo ndiyo sababu,” alisema Kakobe kwa msisitizo.

Askofu huyo alisema, ikibidi Rais Kikwete angefanya uungwana kwa kurejea tena kwa wananchi kwa kuandaa hotuba nyingine ili kuwaomba radhi kwa kuvuruga mchakato huo ndiyo mambo mengine yaendelee.

“Hata kama yeye ni kiongozi, kama amekosea, anatakiwa kuomba radhi…lazima awatendee wananchi haki yao kwa kukiri kuwa yeye ndiye chanzo cha mvurugiko huo ili kuruhusu mchakato wa Katiba uendelee ili Watanzania wapate Katiba wanayoitaka,” alibainisha Askofu Kakobe na kuongeza:

“Sasa umefika wakati wa chama tawala kukubaliana na mabadiliko yanayotokea. Wananchi wa sasa siyo wale wa zamani wakuburuzwa tu. Siku hizi watu wajanja, watu wanataka kuona maoni waliyopendekeza yanafanyiwa kazi bila kuweka usiasa ndani wala si vinginevyo.”

Alisema kuwa juhudi zote za kuunda kamati kwa ajili ya kufanya vikao vya maridhiano ili kutaka Ukawa warejee bungeni zimekuwa zikigongwa mwamba kutokana na kukosa uthabiti juu ya hilo.

Source: Mwananchi
 
Huyu Askofu anapenda siasa kweli....
 
Tafuta tafasiri sahihi ya siasa na katiba, ndipo utajua ni kwa nini kila mtu na mdau wa hivi vitu. Ninahofu kwa tafsiri wrong uliyonayo, inakufanya uone masuala ya katiba ni ya wanasiasa. Big results now!


Huyu Askofu anapenda siasa kweli....
 
Askofu Kakobe naye!
Mwaka 1995 alisimama na Mrema na kummtabiria ushindi!. Mrema aliposhindwa Kakobe kimya!.
Baada ya Ben Kushinda Kakobe aliisupport CCM kiaina.
JK alipoingia Kakobe akaitosa CCM kiaina!.
Wakati wa mgogoro wa nguzo za Umeme aliilaani serikali ya CCM!.

Alitoa waraka kuilaani CCM na kusema ameambiwa na Mungu kuwa CCM haitofika 2015 itakuwa imesambaratika!.

Kuna ukweli ambao wengi hawaujui kuhusu baadhi ya hawa wahubiri wetu, wachungaji wetu,mapadri wetu, maaskofu wetu, mitume wetu na manabii wetu, wengi ni wale Bwana wetu Yesu Kristo aliyewasema "Watakuja watu, watafanya miujiza kwa jina langu,watafanya ishara,watatoa mapepo, wataponya kwa jina langu "kwa jina la Yesu" lakini sio wangu!.
Pasco
 
yupo sahihi mno askofu, anahaki kama kiongozi halafu kama mtanzania!
 
Huyu Askofu anapenda siasa kweli....
Ni kweli lakini hasa anapenda kusifiwa.Sasa tatizo linapokuja, anaangalia wengi wanaoweza kumsifu wako wapi? Zamani waumini waliokuwa wakimsifu walikuwa wengi kuliko sehemu nyingine akajikita kwenye dini hakuhangaika na siasa.

Dini huria zilipoingia na kuongezeka kwa kiwango kikubwa na kusababisha waumini wengi wa kumshangilia na kumsifu kupungua kwa kuhama,waumini kutokujali dini na viongozi wa dini akiwemo yeye akaona ajitose kwenye siasa huko akakuta kuna wa kumsifu kama UKAWA wengi.

Kifupi ni mpenda sifa sana na yuko tayari kujitosa popote kwa gharama yoyote hata kama ni kutelekeza misingi ya dini yake ili mradi asifiwe.
 
Hasira zote hizi, alitaka achaguliwe kuwa mjumbe wa BMK.

Kakobe mtu mzima uthamani,ubora,umaarufu wa BMK huwezi kulinganisha na nafasi ya KAKOBE hata URAIS wa bure hataki sababu ya nafasi aliyonayo Mpe heshima yake
 
Mnyika na mdee wanazoa kura zao nyingi humo,mdee kaongezea na za gwajima pale alipoamua kusakata rhumba lililopigwa na flora michepuko, nakuunga mkono mh kakobe
 
Ni kweli lakini hasa anapenda kusifiwa.Sasa tatizo linapokuja, anaangalia wengi wanaoweza kumsifu wako wapi? Zamani waumini waliokuwa wakimsifu walikuwa wengi kuliko sehemu nyingine akajikita kwenye dini hakuhangaika na siasa.

Dini huria zilipoingia na kuongezeka kwa kiwango kikubwa na kusababisha waumini wengi wa kumshangilia na kumsifu kupungua kwa kuhama,waumini kutokujali dini na viongozi wa dini akiwemo yeye akaona ajitose kwenye siasa huko akakuta kuna wa kumsifu kama UKAWA wengi.

Kifupi ni mpenda sifa sana na yuko tayari kujitosa popote kwa gharama yoyote hata kama ni kutelekeza misingi ya dini yake ili mradi asifiwe.

Pole ndugu,Kakobe anawatu wengi kama kutaka sifa UKAWA ni wachache. KAKOBE mtu makini kama sifa hata sisi tupo humu JF si ili tusifiwe kuwa tumetoa hoja nzuri kumsifia mtu si vibaya.Hata we ukitoa hoja nzuri nitakusifu.Mkeo akikubeza baada ya kufanya jema katika familia utajisikiaje?KAKOBE SHUJAA mpe sifa zake
 
Mtumishi wa mungu anayo nafasi kubwa kuhubiri amani na haki kwa waumini wake,kama haki inapokonywa ni wajibu wake kuzungumza!
 
Back
Top Bottom