Kalenda ya Masomo 2023 inatia ukakasi

Mgimilamaganga

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2019
Posts
271
Reaction score
260
Habari za muda huu wadau wa elimu,bila kupoteza muda nisonge kwenye mada husika;

Nimejaribu kupitia kalenda ya masomo iliyofanyiwa marekebisho,lakini kuna makosa kadhaa yamejitokeza hasa kwenye tarehe za likizo na mpangilio mzima wa vipindi.

Ikumbukwe kuwa kalenda hii imetolewa kama mbadala wa ule waraka uliokuwa unaonesha tarehe za kufunga na kufungua uliotolewa mapema mwezi Disemba na kutumika kuandaa maazimio ya kazi.

Jambo ambalo linawachanganya walimu katika shughuli nzima ya kuandaa namna ya ufundishaji wao kwa mwaka wa masomo husika,kitu kama hiki kilijitokeza mwaka jana pia mara baada ya Tamisemi kutoa kile ilichokiita "Kalenda ya utekelezaji wa mtaala".

Binafsi,ili kuepusha haya,ningewashauri wahusika kuacha kuingilia masuala nyeti kama haya kama hawana utaalamu licha ya kwamba wameteuliwa katika nyadhifa hizo,au wawahusishe walimu moja kwa moja.
 

Attachments

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…