Kaliua Saga: Vita ya Madaraka na uhuni wa wahuni

Kaliua Saga: Vita ya Madaraka na uhuni wa wahuni

kalamu chuma

New Member
Joined
Feb 14, 2021
Posts
2
Reaction score
6
Ulipofika wakati wa kustaafu mzee Nchimbi (the former DEO) watu walitarajia kupata promotion kuchukua nafasi yake lakini haikuwa hivyo badala yake akaletwa Martin Mahinda kushika madaraka ya DEO.

Watu wakaanza kumsoma DEO mpya ni nani na kwa nini kaliua. Kutokana na uchanga wa wilaya nafasi nyingi katika idara ya elimu zilikuwa zinakaimiwa tu hazikuwa na watu walioteuliwa na TAMISEMI muda ukafika ama waliopo warasmishwe km Wana sifa na kama hawana waletwe watu wenye sifa hapo ndipo watu waliporudishwa kufundisha ama kupewa madaraka madogo kulingana na vigezo vyao si Johari pekee yake aliyetolewa na wengine wapo Haina haja ya kuwataja maana si sehemu ya mgogoro.

HUJUMA IKAANZA

Pale kaliua kuna Afisa elimu mmoja Comedian Idara ya sekondary alipogundua status ya mwenzake akaanza kumu-win bwana Martin na kuidhoofisha Idara ya msingi kwa kumfanya mtu wa karibu Sana huku akimhujumu na kuihujumu Idara yake, alitumia uenyeji wake kwa kutaka wateule wengi watoke sekondary na ikibidi wawe wa nyanda za juu hususani Mbeya maana ni mtu wa huko walimu wa sekondary kaliua hili wanalijua vizuri maana km hutoki huko ukuu wa shule utausikia tu labda uwe mwanamke.

Kwa kigezo Cha uenyeji mwamba slishamteka mkurugrnzi mgeni pia hivyo huwa anakaimishwa ukurugenzi kila mara mkurugrnzi anapotoka, Mwamba kakafanikiwa kupendekeza vijana kadhaa kutoka sekondari wakapata uteuzi mzuri kutoka TAMISEMI pamoja na Idara ya msingi kuwa watu wenye uzoefu lakini hawakupata hiyo promosheni na wengine barua zilifichwa. (Bomani hapo haka kamchezo mnakajua na wengine ni waathirika)

Ukaja uteuzi wa waratibu elimu kata. pamoja na vijana wengi kutoka shule za msingi kuwa na elimu inayostahili yule mwamba akafanikisha tena kutungua waratibu kutoka sekondari wa kutosha tena wasiokuwa na uzoefu kabisa na usimamizi wa elimu lengo la mwamba ni kuimarisha Idara ya sekondari msingi watajijua hapa ikaanza kuibuka mining'ono miongoni mwa waratibu juu ya ustawi elimu ya msingi na hilo ndo likaanza kuwa anguko la elimu ya msingi na matokeo darasa la saba kuporomoka maana asilimia 75 ya waratibu wa mwamba wanaishi kaliua mjini huku vituo vyao vikiwa zaidi ya Km90.

Juzi kamalizia na walimu wakuu shule za msingi mwamba katoa ruzuku tena kwa walimu wa sekondari kwenda kuwa walimu wakuu shule za msingi wakati shule za msingi kuna hazina ya vijana wenye ama diploma au shahada wakiachwa. Jambo ambalo linaenda kuua kabisa elimu ya msingi na matokeo ya kaliua yataendelea kuwa duni.

KWA NINI MARTIN MAHINDA? KWANINI VITA YA MADARAKA?

Tukumbuke hapo awali hatukuwa na nafasi ya DEO sekondari ilikuja kuibuka katika mazingira km ya kisiasa na hivi zipo taarifa za kuvunjwa kwa hizi Idara na kurudi kuwa na Afisa elimu mmoja tu kila wilaya mwamba alishaanza kujitayarisha mapema kumuua mwenzake kwa "do or die" maana anamhofia Sana na sababu za kumhofia zipo japo nazo ni hofu zake tu.

Mwamba kafanikiwa totally kumchonganisha Bwana DEO Msingi na Idara yake, waratibu wote, walimu wakuu na walimu kwa ujumla kupitia safi aliyoandaa japo bwana DEO adui yake hamjui kabisa maana kila siku Yupo naye begA kWa bega anamwambia Comred tupambane

KWANINI JOHARI KATIKA VITA HII?
Johari ameanza kufanya kazi na MWAMBA kabla ya Bwana DEO Johari na mwamba wanajuana.

Mwamba kwake kila kinachomuumiza mwenzie ni silaha kwake na hii akaiona itafaa pia kunipigia bwana DEO na kafanikiwa.
Bwana DEO unajua kuna kakundi ofisini kwako hakapo upande wako(na nyie watu wa bomani mnajua hili) na kapo technically engineered na MWAMBA Ila yeye akichochea akiwa mbaali ili bwana DEO asishituke japo wanamuogopa lakini wame-take advantage Haiwezekani Johari APIGWE na MWALIMU MKUU tuhuma ziende kwa DEO tena kwa kurejerea Tukio la zaidi ya mwaka na nusu.

Na JOHARI walimu wanamjua ni mtu wa namna gani waulize watu waliofanya zoezi la BVR jinsi alivyowanyanyasa walimu sasa kakutana na mwenzake Bwana KITINYA(Salary scale haisomi) na yeye akiwa na stress zake kachezeshwa halafu wahuni wametumia advantage za mgogoro kumshughulikia bwana DEO . Ni ujinga kiwango Cha standard guage(hali ya juu).

RAI

Mamlaka zinazohusika imulikeni kaliua mkazione harakati za mwamba na wateule aliojiandalia kwa ajili ya kulinda madaraka yake na harakati za kuua elimu ya msingi kaliua ikiwezekana Bomoeni kaliua yote maana kuanza upya siyo ujinga.

Na kila anayestahili haki na akaipate na anayestahili adhabu naye akanywee kikombe chake.

KALAMU CHUMA

Pia soma;


 
Mwamba umeleta habari mpya,na undani wa chimbuko la Saga ya mwl. kupigwa mabanzi.

Kosa la mwl mkuu kumpiga mabanzi mwl aliyechelewa kazini halivumiliki,mkuu lazima aliwe kichwa mapema iwezekenavyo.

Tuhuma dhidi ya afisa elimu,inaonekana na ma maafisa wenzake ofisini kwake,wapishe uchunguzi.Wapangiwe wakafundishe shuleni (sekondari au msingi) kulingana na taaluma zao.

Wizara iangalie jinsi sahihi ya kupata wasimamizi wa elimu katika ngazi za wilaya na mkoa,tofauti na ilivyo sasa.
 
Mnakoelekea ni KUROGANA mnapenda sana Madaraka
Umenisemea ila nilitaka kuwaambia ulozi, uchonganishi, fitina, unafiki, kujipendekeza, upashkuna ndivyo walivyosomea, hawakufuta ujinga hao wote.

Kiongozi gani anaongoza kwa majungu na umbeya, chuki na roho mbaya.

Ila huko serikalini looh! Bora nishike tu nishike jembe nikalime na kukata mkaa!

Everyday is Saturday............................ 😎
 
Umaskini kitu kibaya Sana, ona mnavyotaka kuuana kisa madaraka!

Kwa maelezo haya sishangai kwanini watumishi mmekuwa wepesi kutumika na wanasiasa.

Haya yote chanzo chake ni dhiki zetu watanzania na ccm ndyo advantage Yao kubwa kuendelea kututawala na silaha Yao kubwa ambayo mi naiita rushwa ni hyo mishahara.

Yaani mtu akilipwa milioni moja anakuwa yupo tayari kufanya lolote atakaloambiwa na watawala ikiwa hta km ni kukiuka haki.
 
Kila niksoma hii hadithi naona giza kubwa la uchawi, ushirikina, ushamba, ujinga na utawala usio wa sheria. Ama naona kamba kambana zimefungamanishwa na mfumo mbovu wa TAMISEMI wa ukosefu wa mfumo sahihi wa kupima performance, mfmo wa hovyo usiokuwa na namna ya kuwabishana na ukosefu wa nidhamu kazini neno ambalo sasa limebaki kama kibwagizo cha siasa na ama kama hazina za visasi ana maonyesho.

Hadi hapo mifumo ya Elimu na miundo ya utendaji kazi katika serikali itakapofumuliwa na kujengwa upya huku tabia za watu kupigwa na viongozi wa siasa ama wateule zitakapokomeshwa, tutegemee vipigo kila siku katika ofisi za serikali, aunyanyasaji kwa wafanyakazi na zaidi sana wateja, majungu na upumbavu mwngi tu kama huu, hautakwisha.

Hata mada nyingi zinazoletwa hapa kuhusu suala hili ni giza tu, maana zinabeba utashi wa mwandishi ambaye naye anamalengo yake kinyume na kundi fulani ndani ya sakata, ingawa ni kweli ofisi ikiongozwa na mtu wa Mbeya, ni kilio kwa makabila mengine. Hilo linajulikanaga kama vile kilimanjaro na bukoba.

Tunasoma watu wamepigwa na viongozi wa kata, wengine wameuliwa katika ofisi za serikali na kukokotwa na pikipiki, mara mkuu wa nini kawapiga walimu mbele ya wanafunzi na mengine mengi. U-FALME WA WAFANYAKAZI WA SERIKALI NA UDHAIFU WA MIUNDOMBINU YAKE SASA NI TATIZO MTAMBUKA KATIKA USTAWI WA TAIFA.
 
Mgogoro huo hauhusiani kabisa na mwalimu Johari kupigwa na mwalimu mkuu.Kupiga mtumishi kwa namna yoyote au chanzo na sababu yoyote haivumiliki kisheria na kiubinadamu.

Tena Kama afisa elimu alimtongoza inabidi afungwe na jela.
 
The Scramble- and Partition for Power in Education Sector A case of Kaliua District in Tabora
Study case.....
Research methodology..... 😂 😂 😂
Wallah unapatia PhD hii thesis!

Everyday is Saturday................................😎
 
Kwahyo mkuu umeamua kutumia ID mpya?

Any way walimu nyinyi mnaongoza kwa majungu na chuki ndio maana mnapelekeshwa sana na mimi siwahurumii hata chembe pasuaneni tu mpaka mpate akili ya kumjua adui yenu ni nani.
 
Kila niksoma hii hadithi naona giza kubwa la uchawi, ushirikina, ushamba, ujinga na utawala usio wa sheria. Ama naona kamba kambana zimefungamanishwa na mfumo mbovu wa TAMISEMI wa ukosefu wa mfumo sahihi wa kupima performance, mfmo wa hovyo usiokuwa na namna ya kuwabishana na ukosefu wa nidhamu kazini neno ambalo sasa limebaki kama kibwagizo cha siasa na ama kama hazina za visasi ana maonyesho.

Hadi hapo mifumo ya Elimu na miundo ya utendaji kazi katika serikali itakapofumuliwa na kujengwa upya huku tabia za watu kupigwa na viongozi wa siasa ama wateule zitakapokomeshwa, tutegemee vipigo kila siku katika ofisi za serikali, aunyanyasaji kwa wafanyakazi na zaidi sana wateja, majungu na upumbavu mwngi tu kama huu, hautakwisha.

Tunasoma watu wamepigwa na viongozi wa kata, wengine wameuliwa katika ofisi za serikali na kukokotwa na pikipiki, mara mkuu wa nini kawapiga walimu mbele ya wanafunzi na mengine mengi. U-FALME WA WAFANYAKAZI WA SERIKALI NA UDHAIFU WA MIUNDOMBINU YAKE SASA NI TATIZO MTAMBUKA KATIKA USTAWI WA TAIFA.
Uko sahihi kabisa, hakuna mfumo wa kuassess performance, Key Performance Indicators, walimu kwenye vyeo wamebakia kujipendekeza, kurogana na kupikiana majungu! Siyo mjini siyo vijijini.

Adui ya mwalimu ni mwalimu..Sad

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mfumo wa kupata vyeo (nafasi) Serikalini hasa huku TAMISEMI ni tatizo kubwa sana.

Hii imewafanya watumishi kujipendekeza mno, kumekuwa na migogoro mingi, Uchama umekithiri mno kama si mwana ccm tena mwana ccm anae wasema vibaya watumishi wasio wana ccm hupat uteuzi.

Kuna ushirikina mwingi sana kwenye hizi ofisi za umma ,nakuhakikishia kuna ushirikina mwingi sana ....watumishi wengi ni washirikina ....period
 
Haya madaraka yatawauweni ninyi watu,hakika kada ya ualimu imejaa watu wanafiki sana,namuomba Mungu Siku moja nihame kwenye hii kada.

Walimu wamejaa kariba ya kujipendekeza kuanzia kwa mkuu wa shule hadi kwa maafisaa wa ngazi za juu kisa kikiwa ni madaraka,ukweli ni kwamba kama uko mtu safi madaraka yatakufuata tuu hata kama utajificha kwenye kona gani,haina.haja ya kulazimisha kuonekana.

Kinachotusumbua walimu wengi ni kutokuwa na shughuli mbadala za kutuingizia vipato,matokeo yake walimu tunakuwa wahanga wa wakubwa zetu kwa kutupelekesha vile wao wanataka, sidhani kama kuna Mwalimu ambaye anaingiza angalau kiasi cha laki tatu nje ya mshahara wake atakuwa tayari kulilia ukuu wa shule au uratibu elimu,maana posho yao ni chini ya laki tatu, walimu wenzangu tujikite kwenye kupambana ili kukuza vipato vyetu na Hizi Vita za madaraka zitaisha.
 
Hivi kaliua siipo nayenyewe tabora? Hakuna maajabu MAJUNGU ndio kwao huko.
 
Mkuu ni kama umeyasema yale nliyotaka kuandika....

Nikiri mimi ni mwalimu, lakini kusema ukweli nawachukia walimu kuliko kawaida .kwa nini?

Walimu ni wanafiki mno, ni watu wenye roho mbaya kuliko maelezo..

Muda wowote mwalimu atakuuza ikionekana anaweza kupata chochote mbele yake..kama kuna kanafas kokote mwal.anaweza kukuchongea ili ukwame...


Walim wengi hasa wenye madaraka hawa wakuu wa shule, waratib wa elimu kata na maafisa elimu...ni washirikina asikwambie mtu....


Nna ushahidi wa baadhi ya wakuu wa shule wanavowafanya walimu wao mandondocha, ili wasihoji chochote kwenye utawala wao...

Itoshe kusema, kila sku nasali na kuomba siku moja nitoke kwenye hii kada...na mtoto wangu ama ndugu kamwe hatokuja kuwa mwalim...MUNGU na aniskie
Haya madaraka yatawauweni ninyi watu,hakika kada ya ualimu imejaa watu wanafiki sana,namuomba Mungu Siku moja nihame kwenye hii kada.

Walimu wamejaa kariba ya kujipendekeza kuanzia kwa mkuu wa shule hadi kwa maafisaa wa ngazi za juu kisa kikiwa ni madaraka,ukweli ni kwamba kama uko mtu safi madaraka yatakufuata tuu hata kama utajificha kwenye kona gani,haina.haja ya kulazimisha kuonekana.

Kinachotusumbua walimu wengi ni kutokuwa na shughuli mbadala za kutuingizia vipato,matokeo yake walimu tunakuwa wahanga wa wakubwa zetu kwa kutupelekesha vile wao wanataka, sidhani kama kuna Mwalimu ambaye anaingiza angalau kiasi cha laki tatu nje ya mshahara wake atakuwa tayari kulilia ukuu wa shule au uratibu elimu,maana posho yao ni chini ya laki tatu, walimu wenzangu tujikite kwenye kupambana ili kukuza vipato vyetu na Hizi Vita za madaraka zitaisha.
 
Mkuu,

Inawezekana na wewe ni mmojawapo ya watu waathirika wa maslahi yaliyohodhiwa na huyo unayemtuhumu. Wewe ni Mbeya (chumvi sokoni) kwa kukamia masuala ya migogoro yenye maslahi binafsi.

Umeharibu unapodaia nakunukuu wewe kalamu chuma" Na JOHARI walimu wanamjua ni mtu wa namna gani waulize watu waliofanya zoezi la BVR jinsi alivyowanyanyasa walimu sasa kakutana na mwenzake Bwana KITINYA(Salary scale haisomi) na yeye akiwa na stress za uchaguzi maana aligombea viti Maalimu wajumbe wakaula makopo bila huruma kachezeshwa halafu wahuni wametumia advantage za mgogoro kumshughulikia bwana DEO. Ni ujinga kiwango Cha standard guage"

Kwa hiyo standard gauge ni kitu kisichofaa? Wewe sio Mtanzania, ni mwongo, una wivu na mchonganishi
 
Back
Top Bottom