CCMkuelekeaUchaguzi
Senior Member
- Aug 18, 2015
- 179
- 77
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt, John Magufuli ameweka bayana sababu za aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu, Juma Kapuya kukatwa na Kamati Kuu ya CCM ingawa aliongoza kwenye kura za maoni za ndani ya chama na badala yake akapewa nafasi ndugu Aloyce Kwezi.
"Kwenye mchakato wetu wa CCM walijitokeza wanaCCM wengi na Kapuya alijitokeza na kuongoza kura na ni rafiki yangu na kaka yangu. Pia alijitokeza Kwezi na mimi ninamfahamu, alipogombea miaka 5 iliyopita hakufanikiwa nikamteua kuwa Mkurugenzi Kilolo. Aliyofanya Kilolo ni maajabu. Amejenga hospitali ya Wilaya; hakuna Wilaya yenya hospitali nzur kuliko Kilolo, ni ya ghorofa. Nikaona kijana ana akili.
Akafufua miradi hadi akaomba pesa za kuunganisha barabara Kilolo na Iringa kwa kiwango cha lami. Nilienda Kilolo kuzindua nikamuuliza kwanini haya usiyafanye Kaliua wilaya inayodorora inakwama na ni ya zamani? Akasema nikienda Kaliua hawanipi kura, wanabadilika badilika.
Ndio maana Kapuya alikuwa wa kwanza kwenye kura za maoni, kwezi alikuwa wa pili wamezidiana kura 8. Kwenye Central Committee tukafanya mabadiliko. Kapuya ni kaka yangu na rafiki yangu lakini miaka imeenda, na ukipata watoto wadogo wadogo unachoka kabisa.
Ingawa ni rafiki na ndugu, nikaangalia nikaona Kaliua inahitaji mabadiliko, spidi mpya ndio maana Central Committee ikamleta Kwezi. Amekuja si kwa makosa, amekuja kuleta mabadiliko ya kweli.
Ndio maana nimewaamini wana Kaliua na moyo wangu umeanza kurudi. Ndio maana tumeshatangaza tenda ya barabara ya Kazilambwa kwenda Malagarasi itundikwe lami.
Ninawaomba mwaka huu msituangushe, kunichagua mimi halafu Diwani na Mbunge wa chama kingine unakuwa umeninyima nguvu za kufanya kazi Kaliua. Mna changamoto nyingi hapa.MNinaomba tushikamane jimbo lisipotee tena. mmejichelewesha sana. Mnalalamika Serikali, mmechagua ninyi, mmechagua wasiochangamana na Serikali.
Hata ukiwa na tochi ukiweka betri usiweke na gunzi ndani, tochi haiwaki. Kwa wanywa pombe ukichanganya gongo na chidugugu na bia na wanzuki mambo yatakuwa mabaya, wekeni chama cha mapinduzi tukafanye kazi kulingana na ilani yetu."