TIASSA
JF-Expert Member
- Jun 17, 2014
- 2,926
- 3,530
Katika kupita pita kwenye mtandao nilikutana na calories calculator hii hapa http://bit.ly/1qDxrrO ambayo, inakokotoa calorie unazotakiwa ule kwasiku hiyo ni kutokana umri ,kilo zako na urefu wako, na kama unataka kupungua kilo moja kila wiki ule calori ngapi kwa siku. Mimi nimekwama sanasana kwenye hiyo kalori tunaihesabuje kwenye chakula chetu tunachokula? Pia uhusihano uliopo kati ya kalori na mazoezi. Kuna watu wamekuwa wakilalamika kuwa pamoja nakufanya mazoezi wamekuwa badala ya kupungua unene unaongezeka tu. Asanteni naomba mwenye uelewa juu ya haya makitu tuelimishane..