Kama adhabu ya Ali Kamwe ni miaka miwili, Kamati ya Nidhamu haina nidhamu wala maadili. Mmetia aibu taarifa kutoka nje kabla hamjaweka wazi

Kama adhabu ya Ali Kamwe ni miaka miwili, Kamati ya Nidhamu haina nidhamu wala maadili. Mmetia aibu taarifa kutoka nje kabla hamjaweka wazi

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Naangalia channel tena. Mchambuzi mmoja anasema kama kweli adhabu ya Ali Kamwe itakuja rasmi miaka miwili basi hii kamati haina nidhamu, Maadili na Hekima.

Haiwezekani kamati hawajatangaza rasmi adhabu lakini taarifa imeshavuja Nje. Hili suala TFF mkajitathimini, mkakajiangalie madhaifu yenu. Mimi nawasubiria mtoe taarifa rasmi ntawachamba kweli.

Ole wenu iwe miaka miwili.

Yaani humo kwenye kamati wote mnakuwa wambeya na wanafiki. Hamna madili wala NIDHAMU. Kama taarifa zenu zinaweza kuvuja kabla amjatoa taarifa rasmi mjue mna shida.

Na shida kama hizi ndizo Ali Kamwe anawaonya mbadilike.

Mkiambiwa mbadilike hamtaki mnatishia kufungia watu.

Mungu atawahukumu na mtatatia aibu milele soka letu.
 
Zinavuja siri za serikali ndiyo ije kuwa kikamati cha TFF. Karani aliyepewa kazi ya kutype taarifa anaweza pia kuvujisha.

TFF wanapobadilika wasisahau pia kutupia jicho ule udhamini wetu pendwa wa timu 8 unaoipa timu fulani ubingwa wa mbeleko.
 
Watu wakishakutana baa wakapiga bia 2 tatu wa karibu mtajua tu ni wakina nani na wana mipango gani
 
Back
Top Bottom