Unahisi hao askari ndio itakuwa bora?
Hujawahi ona matukio ya askari na raia mitaani?
Hawa askari wa TPDF unaosemea hawajajifunza kulinda wanyamapori, ni wastage of resources
Hao askari wa hifadhi hiyo ndio kazi yao, wamesomea hiyo hakuna sababu kuwaondolea jukumu lao sema wabanwe wafanye kazi kwa weledi, tatizo la nchi hii watu wanapenda mno kutumia madaraka yao kuonea wenzao, sio polisi wala migambo wala mahakimu!
Mkuu usipende sana kila kitu kifanywe na askari, naona siku hizi wanaingia kwenye kila kitu kuanzia siasa hadi mambo ya kiuchumi. Hii si sawa. Tuwaachwe wabakie makambini waendelee na majukumu yao