Kama bado unapenda kuendelea kupigwa hela kwenye shule za EMs , usiwafokee wazazi wanao warudisha watoto Kayumba Kwa sababu wenzako wameshajielewa

Kama bado unapenda kuendelea kupigwa hela kwenye shule za EMs , usiwafokee wazazi wanao warudisha watoto Kayumba Kwa sababu wenzako wameshajielewa

Bongotunacheza

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2018
Posts
983
Reaction score
2,306
Kasi ya wazazi kuwatoa watoto Wao shule za EMs kuwarejesha Kayumba inazidi kuongezeka kila siku.

Huko mtaani ni balaa mamia Kwa maelfu ya wazazi wanawatoa watoto Wao shule za EMs na kuwarudisha Kayumba.

Tayari wamesha jielewa. Tayari wamesha jua walifanya makosa. Na hawataki kufanya makosa Tena.

Cha ajabu baadhi ya wazazi hao wanapokuja hapa jamvini kushare Kwa wazazi wenzao furaha ya kufanya maamuzi mazuri kwenye maisha Yao wanajitokeza wazazi wanaosomesha Ems na kuwaambia " Huna hela" una stress nakadhalika.

Acheni hizo Bana. Kuwa na hela haimaanishi ndio uzitumie kijinga kijinga.

Wazazi wengi wanao somesha Ems ni masikini tu kama wazazi wanao somesha Kayumba. Wanao somesha international schools za mtaala wa Cambridge hao ndio wana uwezo.

Mzazi alie hamisha mtoto wake Ems na kumleta Kayumba anapo leta Uzi hapa ni moja ya relief Kwa pesa nyingi alizo poteza Ems.
 
Na wewe ukiwa unawarudisha huko kayumba usijitambe kuwa umeshajielewa kila mtu ashinde mechi zake🫵🏿
 
Kikubwa kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake,

No, kukejeliana
 
Hao ni wale waliojishaua kuwapeleka wtt ems huku hawana kazi..wala biashara za kuweza kuwasupport kulipa gharama...mtoto killa siku anaachwa na gari au anatolewa nje...wameona wanaumbuka....ila kama wazazi wamejipanga vzr na wana huo uwezo wa kulipa shida iko wapi?
 
Hao ni wale waliojishaua kuwapeleka wtt ems huku hawana kazi..wala biashara za kuweza kuwasupport kulipa gharama...mtoto killa siku anaachwa na gari au anatolewa nje...wameona wanaumbuka..

Wanaunda asilimia 90 ya wazazi wanao somesha Ems
..ila kama wazazi wamejipanga vzr na wana huo uwezo wa kulipa shida iko wapi?

Hakunaga.

Wazazi wenye uwezo wanasomesha International Schools ( Mtaala wa Cambridge) Ada Dola elfu 30 Kwa mwaka.

Wanao somesha Kayumba wote ni hohehahe
 
Kama kuna kipindi ambacho wazazi wanapaswa kuwapeleka watoto wao shule za English Medium basi wakati huu ambapo mtaala mpya umekuja kuanza ndio sahihi zaidi.
 
Back
Top Bottom