Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Polisi wanasema waliyazuia maandamano ya Chadema, yaliyotakiwa kuwa ya amani, kwa sababu walikuwa na habari za intelijensia kwamba Chadema walikuwa wamepanga kufanya vurugu. Sawa, kama ni kweli Polisi walikuwa na haki ya kuyazuia hayo maandamano.
Lakini sasa, kwa kuwa maandamano ni haki ya kikatiba ya Chadema, kama Polisi wameibuka tu na kutoa visingizio na sababu za uongo katika kuzuia maandamano, labda kwa sababu kulikuwa na amri toka juu, kitu gani kinawazuia Chadema kwenda Mahakamani kuwafikisha Polisi (hususa IGP na Waziri wa Mambo ya Ndani) mahakamani, na hata kuwadai fidia?
Kwa nini Chadema wasiende mahakamani ili Polisi waotoe ho ushahidi na kuiridhisha mahakama kwamba kweli Chadema walipanga kufanya fujo ndio maana wakayazuia maandamano?