Kama "Corona virus spread" itaendelea kwa Kasi hii Ulimwenguni! Nadhani Ni muda muafaka, serikali kusuport biashara ya Forex

Thailand

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2019
Posts
275
Reaction score
795
Ndugu wafanyabishara na wajasiriamali wenzangu poleni kwa magumu yanayokumba biashara zenu hasa kipindi hiki Cha Corona virus. But on other side nipende kuwapa pongezi wajasiriamali wengine wanaokula sahani moja na hii outbreak ya Corona kwa maana kwamba wanatengeneza faida kutokana na ugonjwa huu wa Corona.

Nipende to kusema kwamba kinakuja kipindi kibaya kabisa katika historia ya mwanadamu. Yaani kutokana na Corona tutegemee watu kuzuiwa kutoka kwenye miji yao ikiambatana na mazuio ya michangamano na mikutano. (No physical market interaction, No physical political crowds, no physical church worship, no physical motivational speaking crowds etc)

Ni jikumu la sisi sote kuona kwa macho ya kipekee juu ya Nini kifanyike kwa wakati gani ili kunusuru suala zima la kuwezesha maitaji ya wanadamu.

Huwezi kupata maitaji yako muhimu Kama chakula, malazi na mavazi Kama huna pesa. Na mfumo rasimi wa kupata pesa Ni either kuajiriwa au kujiajiri ambapo traditionally tumezoea kupata vitu hivyo kwa direct contact Kati ya mtu mmoja na mwingine kitu ambacho mwisho wa siku kinatengeza crowd ya people kwenye eneo moja.

Mfano mzuri cheki masoko Kama ya kariakoo n.k namna watu wengi wanavyojipatia hapo riziki yao.
Sasa umeshafikiria mkusanyiko mkubwa Kama huo na masoko mengine Tanzania nzima pindi utakapozuiwa kuepusha maambuzi ya corona hivi unafikiria watu watakuwa kwenye hali gani? Haya wewe mwajiriwa pindi utakapozuiwa Ishmael kutohudhulia kazini ili kupunguza maambukizi ya virus vya Corona wewe umejipangaje.

Pale kwenye club ya FC Barcelona wachezaji wameombwa wakubali kupunguza a mishahara yao kuepusha time isiingie kwenye madeni makubwa kwa sababu Sasa hivi haingizi pesa za kutosha. Ikikutokea hii umejipangaje kwa sababu tumaini la mwajiriwa daima Ni kusikia amepandishiwa mshahara.

Kwa hivyo ipo changamoto kubwa duniani hasa kwenye sekta ya biashara na uchumi. Katika kuwaza waza kwangu kuhusu hali inavyoweza kuwa baadae ndipo nikaona biashara iliyo safe kwa mtu yeyote kwa kipindi hiki Ni Forex. Nasisitiza Tena biashara itakayo kuwa safe kwa mtu yeyote Ni Forex kwa sababu utaweza kuifanya hata ukiwa chumbani kwako au umefungiwa karantiini.

Ni biashara utakayoweza kufanya kwa simu yako au computer Kama unayo. Ni nzuri kwa maana hata Kama duniani (major pair) kutakuwa na hali mbaya kwa pair hizo wewe uta sell hizo pair na bado kwa upande wako ukatengeneza faida. Hali ya hizo pair Kama itakuwa nzuri uta Buy hizo pair na kupiga faida pia.

Sasa nilikuwa naomba serikali iingilie Kati hii biashara ili ieleweke vizuri kwa watanzania wengi waweze kujiajiri pindi Mambo ya lockdown yanapoweza kuigia katika nchi yetu. Tatizo la serikali yetu Ni watu waliolala Sana kwenye Mambo ya kisasa wao huamini katika ushirikina na kukomoa wapinzani. Lakini vitu vinavyoweza kuleta manufaa kwa watanzania wengi Wala hawavijali. Ndo maana zaidi ya miaka 50 tunatumia katiba tulioachiwa na mkoloni. Mfumo wetu wa Elimu mbovu lakini viongozi wapo SIJUI kwa maslahi ya Nini.

Rasimisha vitu vinavyoweza kuwa na msaada mkubwa kwa watanzania. Mfano hakuna broker mtanzania kwenye biashara hii ya Forex hali Kuna watanzania wengi wanaojihusisha na biashara hii serikali haioni hizo Ni pesa zake zinaenda nje ya nchi.

Simamia ma broker au au serikali ianzishe broker company yenye nguvu humu humu ndani kwa ajili ya kufanya biashara na Forex trader wote wa Tanzania. Broker atake saidia kutoa Elimu makini juu ya foreign exchange market kwa watanzania. Serikali kutokuwa serious kwenye Mambo ya msingi ndio maana watu wachache wanatumia udhaifu huo kuwaibia watanzania.

Yapo mengi ya kuelezea Ila Forex ikipata back up ya kutosha kutoka serikalini inaweza kuwa msaada mkubwa kwa watanzania wengi.
 
Serikali ilishaipigaga marufuku iyo biashara ya forex,Iyo ni kama ni kamari tu
 
Kwahiyo kila mtu akianza kufanya hiyo Forex mtakula nini ?

Mko obsessed na pesa mpaka hamjielewi.

Forex doesn't add any value to human life.

Hivi kama kukiwa na upatikanaji wa mabilioni yasiyohusiana vyovyote na HUDUMA au BIDHAA fulani yanakuwa na VALUE gani hasa ?
 
mbona tunawaambia hizi biashara za Internet ni WIZI mtupu? na hasa FOREX
huwezi kaa kwenye Laptop ukawaibia wenzako tafuta shamba berega panda nyanya vuna upate pesa
mwaka huu hakuna ujanja ujanja
 
Nlifikiri utasema kuwa sasa ni muda muafaka serikali kuruhusu watanzania kuweza kupokea pesa kwa njia za mitandao kama Paypal ili kuwezesha biashara za mitandaoni kumbe unapigia debe kuwatapeli watanzania kwa Forex!! 😀

Sasa watu wakishaweza kuexchange pesa mtandaoni na kupata mabilioni, watakula izo pesa za forex?
 
vijana mmewehuka sana fanyeni kazi hizo Forex zenu utapeli mtupu mkamatwe mpigwe selo kabisa Mali inapatikana shambani
 
Nadhani forex ijumuishe biashara zote za mtandaoni (online business and marketing)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…