voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,545
- 11,935
Kwamba Mheshimiwa Rais anapongezwa kwa kuifungua Demokrasia nchini. Lakini maandamano ya kupinga Ufisadi, Ubadhirifu na hujuma zilizotajwa na CAG yakipigwa marufuku?
Kwamba Serikali inayopinga ubadhirifu,ndio hiyohiyo inayozuia maandamano ya wananchi kuipongeza kwa kuyaibua hayo madudu kupitia ripoti ya CAG na kuyatangaza hadharani?
Hivi Demokrasia iliyofunguliwa ni ipi? Ya ushirikiano wa kulamba asali bila kupingana hadharani?
Ya kuitana kwenye tafrija na kujazana mapambio ya kusifiana?
Hivi ina maana mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, naye hajasikia kwamba maandamano ya ACT yamezuiwa na Polisi?
Na kama alisikia na kukaa kimya kwa jambo nyeti kama hilo,ni nini tafsiri yake?
Tukisema hakuna jipya ndani ya utawala huu,dhidi ya wafujaji wa mali za umma!
Bado mtaendelea kutuita Sukuma Gang?
Haya bhana, mi napita tu!