Kama hakuna tatizo, kwanini wanataka maridhiano?

Kama hakuna tatizo, kwanini wanataka maridhiano?

Mtemi01

Member
Joined
Dec 23, 2023
Posts
18
Reaction score
35
Kwa nyakati kadhaa viongozi wa serikali na CCM wamekuwa wakisema nchi Iko shwari, watu wako huru wanafanya siasa zao bila shida. Yani kiufupi hakuna tatizo lolote.

Lakini watu hao hao utasikia 4Rs, mara upinzani walikataa maridhiano. Na hivi karibuni Mzee Wasira amesema wao wako tayari kwa maridhiano.

Swali ni je, ni maridhiano gani huongelwwa hapa? Yani hakuna tatizo lakini tunataka maridhiano, ya Nini? Mi nijuavyo ukishasema upon tayari kwa maridhiano maana yake umekiri kuwepo kwa tatizo.
 
Logically uko sahihi mkuu,cha kujiuliza ni kuwa mbona CHADEMA inawanyima usingizi namna hii?
 
Ukiuliza maswali magumu kama haya ccm watakupa majibu mepesi
 
Back
Top Bottom