Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,762
- 59,204
Mwaka 2005 mzee wangu alikuwa haabiwi lolote juu ya Kikwete. Alidiriki hata kumpigia kampeni nyumbani kwetu na hata kwa majirani. Hakutaka kumsikia mtu yeyote akiongea jambo lolote baya juu ya JK. Kwa kifupi mapenzi yake kwa CCM na JK yalikuwa motomoto.
Tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi wa mwaka huu nikaona si vibaya nikafunga safari kwenda kumtembelea mzee na kumsikiliza msimamo wake juu ya Kikwete na chama chake.
Kama kawaida nilijua mzee bado hapendi kusikia ubaya wowote wa CCM na hivyo ili nisimuudhi nikaona ni bora nianzishe mada kwa kumsifu Kikwete na chama chake kuwa wametekeleza ahadi nyingi walizoahidi kipindi kile. Nilianza kwa kusema 'Mzee, hivi hapa kampeni zinaendeleaje maana kule mjini ni kivumbi na jasho ila tunamwamini rais wetu Kikwete atashinda maana kutekeleza ahadi karibu zote alizotoa kipindi kile'.
Sikuamini nilichosikia kuto kwa mzee wangu. Akasema kama umekuja kwa ajili ya kumpigia kampeni Kikwete, hapa umepotea njia na inawezekana labda ulikokuwa ukienda bado haujafika hivyo tuulize ni wapi ili tukuelekeze.
Nilichanganyikiwa ikabidi niwaulize taratibu waliokuwa karibu kilichomsibu mzee na nilichoambiwa ni kwamba mzee hivi sasa hataki kusikia kitu chochote kinachohusiana na Kikwete na chama chake. Na kweli mzee wangu kaweza kubadilisha watu wengi tu ikiwemo na majirani zake.
Nilifurahi sana kusikia hivyo na nikamwambia kuwa nilikuwa namsanifu tu, ndipo tulipoanza kuongea lugha moja, yaani mwaka 2010 HATUDANGANYIKI
Ndio maana ninasema kama mambo yenyewe ndo hivi basi Dr. Slaa asubiri kuapishwa tu maana kama ushindi tayari amekwisha upata.
Post of the year to me.Nahisi kupona ugonjwa nisioujua very soon
Mwaka 2005 mzee wangu alikuwa haabiwi lolote juu ya Kikwete. Alidiriki hata kumpigia kampeni nyumbani kwetu na hata kwa majirani. Hakutaka kumsikia mtu yeyote akiongea jambo lolote baya juu ya JK. Kwa kifupi mapenzi yake kwa CCM na JK yalikuwa motomoto.
Tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi wa mwaka huu nikaona si vibaya nikafunga safari kwenda kumtembelea mzee na kumsikiliza msimamo wake juu ya Kikwete na chama chake.
Kama kawaida nilijua mzee bado hapendi kusikia ubaya wowote wa CCM na hivyo ili nisimuudhi nikaona ni bora nianzishe mada kwa kumsifu Kikwete na chama chake kuwa wametekeleza ahadi nyingi walizoahidi kipindi kile. Nilianza kwa kusema 'Mzee, hivi hapa kampeni zinaendeleaje maana kule mjini ni kivumbi na jasho ila tunamwamini rais wetu Kikwete atashinda maana kutekeleza ahadi karibu zote alizotoa kipindi kile'.
Sikuamini nilichosikia kuto kwa mzee wangu. Akasema kama umekuja kwa ajili ya kumpigia kampeni Kikwete, hapa umepotea njia na inawezekana labda ulikokuwa ukienda bado haujafika hivyo tuulize ni wapi ili tukuelekeze.
Nilichanganyikiwa ikabidi niwaulize taratibu waliokuwa karibu kilichomsibu mzee na nilichoambiwa ni kwamba mzee hivi sasa hataki kusikia kitu chochote kinachohusiana na Kikwete na chama chake. Na kweli mzee wangu kaweza kubadilisha watu wengi tu ikiwemo na majirani zake.
Nilifurahi sana kusikia hivyo na nikamwambia kuwa nilikuwa namsanifu tu, ndipo tulipoanza kuongea lugha moja, yaani mwaka2010 HATUDANGANYIKI