Kama harusi imehairishwa ni vema nikadai mchango nilioutoa?

Kama harusi imehairishwa ni vema nikadai mchango nilioutoa?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Naombeni ushauri wakuu kama mnavyojua tarehe mbaya hizi hapa nilipo nimenasa haswa Sina hata mia yaani ikitokea ghafla bill ya maji au umeme naaibika maana kila ninayemgusa analia njaanuary kapeleka watoto shule.

Back to the topic Kuna group letu la shule kuna jamaa yangu tumemchangia mchango wa harusi toka mwaka jana Ila harusi yenyewe Imeingia kiwingu Mara sijui imehairishwa sijui Mara sijui watatutangazia Tena Kama itakuwepo mwishoni mwa mwaka huu nahisi wamefumaniana au Kuna mgogoro upande wa wazazi hivyo hakuna uhakika wa harusi kufanyika admin mwenyewe hapewi ushirikiano Tena hivyo hatupi updates.

Sasa Mimi roho inaniuma Sana nilijifanya muhamasishaji nikatoa 50000 yangu kumchangia hapa nilipo naitamani kweli hio pesa Ila nashindwa niidai kwa style gani naona Kama afisa nitajizalilisha ndo nawaza hapa niipotezee tu au nianze kampeni ya kimyakimya niwahamishe member wenzangu katika inbox tuliochanga kumdai huyu bwana harusi miyeyusho kweli.Aisee Kama huna hela kuishiwa kubaya Sana yaani utawaza pesa zote za nyuma ulizowapa watu offer au kuwasaidia.

Nashauri tunaotegemea mishahara tujaribu kuwekeza kwenye biashara hata ndogondogo ili tarehe Kama hizi hudati unachomoa hata 20000 kwenye biashara inakusogeza.
 
Kuna mwamba tumlichangia ofsin akasepa na hela zetu.hatukuona Ndoa wala mtoto wa ndoa

Jamaa akawa mkavuu kama hakuna kitu kilitokea vile
 
Hii ni moja ya sababu hufanya kuchangia sherehe hususan harusi kuwa vigumu sana
 
Kuna mwamba tumlichangia ofsin akasepa na hela zetu.hatukuona Ndoa wala mtoto wa ndoa

Jamaa akawa mkavuu kama hakuna kitu kilitokea vile
Huyo jamaa ni ana akili ka zangu, safi sana[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kama ulivyo hamasisha michango hamasisha tena mdai hela zenu.
 
Hizo soda na bia ulizokuwa unakunywa wkt wa kamati unadhani imetoa wapi
 
Hapo mmepigwa andikeni maumivu tu, non refundable...jamaa kashajipatia mtaji kwa ndoa ya mchongo
 
Back
Top Bottom