Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 26,961
- 77,890
Wadau wa JF Garage.
Kuna chuma, EV kutoka kampuni la Kijapan Mitsubishi inaenda kwa jina Mitsubishi i-MIEV (Mitsubishi innovative Electric Vehicle).
Hii unaweza kuipata BEforward kwa bei kati ya Mil 5 hadi 6 na kuendelea, na kodi zake (kwenye calculators ya TRA haipo) nimeulizia ni Tsh Mil 3.5 tu. Kwa makadirio bei jumla ni Mil 9-10.
Ni kagari flani kana design ya kipekee kama mitoko ya Madonna, na ukipita mahala lazima watu wageuze shingo. Ila muonekano ni subjective, kila mtu ana mapendeleo yake. Tuje kwenye specifications.
Kama tulivyosema ni EV yenye range ya 160 kilometa, kutoka kwenye battery ya 16kWh inayoisukuma motor yenye 47 kW (63hp). Ina port mbili za kuchaji, ya kawaida AC Level 1 ambayo inataka 15A na 110-240V unaweza chajia ata nyumbani na Fast charger DC.
Ni hatch yenye milango minne, design yake kidogo ina utata especially kwenye matair, ya mbele na nyuma hayafanani size, hii tuwaachie mainjinia wa Mitsubishi na badala ya spare tyre wanakupa compressor ya 12v utayoiplug kwenye cigarette lighter.
Maisha ni kujilipua.