Kama hauwezi kulipia VPN Tumia TOR circuit bure kama mbadala

Kama hauwezi kulipia VPN Tumia TOR circuit bure kama mbadala

kali linux

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2017
Posts
2,192
Reaction score
5,685
Hello bosses

Kwa hali ya sasa kumekua na wimbi la watu kukimbilia VPN ili kuaccess internet kwa wanaopata shida ya internet breakdown. Kutumia VPN kuna madhara yake ukiachana na slow speed kwa baadhi ya VPN providers.

Madhara makubwa ya kutumia VPN ni kwamba VPN provider wako anaweza kuona kila data zako unazotuma na kupokea hivyo akitaka kujua umesurf nini ni rahisi kwake kufanya hivyo. Kwa wanaotumia apps au websites ambazo hazifanyi end to end encryption au hazina ssl wako kwenye hatari zaidi ya kuingiliwa kwenye mawasiliano yao, kuibiwa passwords etc......

Kwenye dark web kuna hackers huwa wanatoa password dumps zinazokuwa zimebeba passwords zinazotumika mara kwa mara na moja ya chanzo cha hizo data huwa ni passwords zinazotumwa kwenye websites ambazo hazina ssl (requests & data sent or received to/from the server are not encrypted) pamoja na data kutoka kwenye VPN(hasa free VPNs).

Pia VPN providers wana uwezo wa kuuza data zako bila wewe kujua.

Suluhisho la hii ni kutumia TOR circuit. Sitoelezea kiundani sana ufanyaji kazi wa tor circuit lakini kiufupi ni kwamba request yako inapitishwa kwenye nodes mbalimbali kabla ya kutoka na kuingia kwenye exit node yako. Hii ni tofauti na VPN za kawaida kwa sababu kwnye VPN unakua umepewa Server moja ifanye kazi kama intermediary wako, so ni kama vile unaiambia server ikutafutie kitu fln au i-fanye login sehemu fln etc..... Kwa TOR circuit request yako haitofuata route moja bali requests tofauti zinaweza kufuata routes tofauti ila zikawa na exit node moja ambayo ndio inakulink ww na TOR circuit, hii inaondoa uwezekano wa requests zako kuwa logged sehemu moja kama ilivyo kwa VPN

UNAJIUNGAJE NA TOR CIRCUIT.?
Kwa wenye smartphone kuna app inaitwa ORBOT Tor, na pia nadhan kuna windows version yake. Download kisha weka kwenye kifaa chako na itakuuliza ku-enable 'Built in VPN', iruhusu kisha utachagua apps zipi zitumie TOR circuit. ORBOT TOR ni rahisi kutumia na inajieleza.

Kwa wanaotumia parrot OS kujiunga na TOR circuit ni kitendo cha 'one-click; tu. Fungua menu kisha chagua 'Anon-surf' then 'Start Anon-surf'

===============>
UPDATE

Kwa wanaotumia windows ukiweka TOR browser itakuconnect moja kwa moja na unaweza kuitumia kufungua web ambazo hazipatikani kama youtube na jf

============>

UPDATE 2

Maelekezo na link ya orbot App yapo kwenye hii comment

Post in thread 'Kama hauwezi kulipia VPN Tumia TOR circuit bure kama mbadala' Kama hauwezi kulipia VPN Tumia TOR circuit bure kama mbadala

========>

NOTE:
WATU WENGI HUHUSISHA TOR NA DARK WEB LAKINI TOR CIRCUIT INAWEZA PIA KUKUSAIDIA KU-BROWSE INTERNET ANONYMOUSLY NA KUEPUKA USUMBUFU WA KUTOINGIA KWENYE APPS AU WEBSITES AMBAZO ZIMEZIMWA KWENYE ENEO ULIPO. SO TOR CIRCUIT HAITUMIKI KWA DARK WEB TU LAKINI NI ALTERNATIVE NZURI YA VPN

Happy Surfing!
~Kali Linux
 
Hivi naweza kulipia data za VPN na nisinunue data za hizi kampuni za simu?

Mfano, VPN nayotumia imenipa GB 20 bure, nimetumia zimebakia 7, wamasema nilipie 20k unlimited mwezi mzima.

Je nikinunua hiyo unlimited sihitaji kununua za mtandao naotumia?

Kuna vitu vinanichanganya wataalamu mnipe msaada wa maelezo.

Ahsante.
 
Vpn gani hiyo ya kupewa GB za bure
 
Hivi naweza kulipia data za VPN na nisinunue data za hizi kampuni za simu?

Mfano, VPN nayotumia imenipa GB 20 bure, nimetumia zimebakia 7, wamasema nilipie 20k unlimited mwezi mzima.

Je nikinunua hiyo unlimited sihitaji kununua za mtandao naotumia?

Kuna vitu vinanichanganya wataalamu mnipe msaada wa maelezo.

Ahsante.
Mkuu wote wanatumia neno data lkn wanamaanisha vitu viwili tofauti
1)Data (Context ya Kampuni za simu)
-->hiki ni kiasi cha information ambacho unaweza kutuma na kupokea ndani ya wakati fln kwenye mtandao. Mfano natumia voda na nikanunua gb1 kwa siku, hio inamaanisha kwamba naruhusiwa kupokea na kutuma data kupitia internet zenye jumla ya size ya 1gb, nikizidi hapo huduma ina-stop. Na hii aina ya data bundle ndio inakufanya upate huduma ya internet. Sasa inategemea na jinsi utakavyo taka kuaccess hio internet yako. Kama utataka ku-access ukiwa anonymous (yaani unataka kudanganya sehemu ulipo ili upate huduma ambazo hazipatikani mahali ulipo kiuhalisi) basi itabidi utumie VPN au TOR ila kama unataka ku-access kawaida tu basi hamna haja ya VPN ama TOR. Tuseme umeamua kutumia VPN, next naelezea data upande wa vpn

2)Data (Context ya VPN)
--->Hapa kwanza inabidi ujue vpn inafanya vipi kazi. Kiufupi vpn ni kama intermediary kati yako na website au huduma zinazopatikana kwa intaneti. So kama unatumia vpn kufungua google.com basi hauendi moja kwa moja google.com lkn unaiomba vpn server yako ikufungulie google.com kisha yenyewe itafungua na kukutumia wewe, hio process yote inahusisha utumaji wa data. Na hapo wanapokwambia ununue data za VPN basi wanamaanisha kiasi cha data ambacho unaweza kuiomba VPN server ikutafutie na kukutumia. Hii Pia inatokana na pricing feature ya VPN husika. Kuna VPN zinatoa price kutokana na data unazo-transfer lkn kuna VPN zinatoa price kutokana na muda utakaotumia eg 1 week, month etc...

So kiufupi kabisa kama haujaelewa hapo juu ni kwamba hata kama ukiwa na Data bundle za kwenye vpn ila kama hauna za kwenye mtandao wako wa simu hautoweza kupata internet coz za kwenye mtandao wa simu ndizo zinakufungulia internet afu ni juu yako sasa jinsi ya kuaccess hio internet uliopewa.
 
Mkuu ujue hapa you are dealing with an illiterate person kwenye haya mambo hivyo nivumilie kwa maswali yangu ya kijinga.

Kwa hiyo hata kama natumia VPN siwezi kupata mtandao ama kupata access ya mitandao bila kwanza kununua data kutoka kwenye mtandao wangu?

Sasa iwapo nina data za kwenye mtandao wangu, za kwenye VPN ni za nini?
 
kwenye VPN ni za nini?

Mkuu kaelezea vizuri sana hapo juu, labda nikazie tu

1. gharama za ISP wako ( eg: Tigo, Voda ) kwa ajili ya data aka bando

2. gharama za VPN provider kwa ajili ya data aka bando

so long as unatumia VPN , izo gharama 2 uwe tayari kuzimudu, maana unatumia kompyuta ya mtu mwingine ku surf web zilizokua blocked kwenye nchi yako

ujue kitu kimoja, unapotumia VPN, kuna server ( server ni kompyuta kubwa ) ya jamaa iko ON uko kwingine ( nchi nyingine ) , iyo server inahitaji umeme, internet , etc, so wewe ndio unakava izo gharama

VPN hazina uhusiano wowote na ISP wako,

hata wewe hapo unaweza launch VPN yako , so watumiaji inabidi wachangie gharama za uendeshaji,

kuna VPN za free, ila zina limit pande wa speed na data

kama ni paid VPN ( yakulipia ), inabidi wakuchaji kwa matumizi ya bando ukave running cost ya server

a. kwa Volume basis, say: 1GB kwa sh.100 au

b. kwa Time basis , say kwa mwezi mzima ni sh. 20k

so lazima ununue data kutoka kwa ISP then kisha lazima ununue kutoka kwa VPN provider ( kama ni paid one )

NB: na assume loopholes (za ports) za ISP zipo okay
 
Ma programmer wa Tanzania Mpaka sasa wameweza nini? Au ujuzi wao ndio uneishia kutengenezwa tu vi app vya kuchezea?
Vpn za Tanzania pia zipo, sema vpn na wao pia wanaunga bando kama sisi, ukiweka vpn ya Tanzania wewe unatumia Voda na Vpn inatumia TTCL itakusaidia nini?

Ndio maana watu wanaweka vpn za Nje ambazo zinatumia bando za nje.
 
Naomba kwa anaejua kuset vpn configuration kwenye ios anisaidie wakuu
 
Nitumie basi mzee

1.nenda setting
2.then general
3.then vpn
4.then click add vpn configuration
5.then after kwenye type unachagua ya mwisho L2TP
5.then kwenye description andika vpn
6.then kwenye server write this code 219.100.37.180
7.kwenye account write vpn
8.password again andika vpn
9.kwenye secret again andika vpn
10.after filling all this unabonyeza done kwajuu
11.itakuja status unabonyeza on
Note:Make sure your mobile data is on na una kifurushi
 
Kwenye android tunafanyaje mkuu
 
Nitumie basi mzee

Nitumie basi mzee

IMG_1748.png

Kama hapo
 
Back
Top Bottom