Kama hewa itatoka katika eneo lililo na uwazi, je ni kitu gani huzuia hewa isitoke nje ya uso wa dunia?

Lakini hapawezi kuwa na mgandamizo pasipokuwa na kingo au vizuizi
Umetaja pointi ya maana sana ambayo nina hakika huielewi kikamilifu. Ni kama vile umeitema kibahati nasibu.

Kinachosababisha shinikizo au mgandamizo wa hewa au chochote kile ni kani mvutano ambayo hukifanya kitu hicho kuuzonga uso wa dunia.

Ukingo au kizuizi hapa ni uso wa dunia ama ardhi ambayo hewa au maji au chochote hukandamiza.

Wakati hewa yenyewe, mathalani, inaishinikiza dunia kwa sababu ya uzito wake, dunia nayo (kizuizi/ukingo) huisukuma hewa kuelekea juu.

Hii ni kwa mujibu wa sheria ya tatu ya mwendo au mjongeo ya Newton.

^Kwa kila tendo kuna mwatuko wiani na ulio kinyume chake.^
 
Haya tushamwambia muda mrefu lakini ni mbishi
 
Kama ukingo ni uso wa dunia, ukingo mwingine wa upande wa juu ni upi?
 
Hizo fact ndizo bado sijazielewa na kuziamini
Kama ipi huamini mkuu???
Chukuwa waya uweke karibu na sumaku alafu pitisha umeme kwenye waya utaona waya unasukumwa/kuvutwa. Charged particle yoyote ikimove katika sehem yenye magnetic field inakutana na force, hii application utaiona hata kwenye mota
Gravity sihitaji kusema mengi unajuwa kama ipo.
Kuhusu diffusion, jaalia umepuliza pafyumu hapa na pembeni kuwe na jiko linatoa mvuke halafu zote zisambae utaona pafyumu itasambaa fasta chumba kizima kabla ya mvuke kwasababu ni less denser kwahiyo inadiffuse faster
 
Sijaelewa swali lako
CD si imekaa kwamba ukiiweka sehem kuna sehem unaanzia kushoto hadi kulia? Sasa tusaidie kutuambia ni nchi gani iko kushoto na ipi iko kulia mwa Dunia?
Na hiyo nchi iliyoko kushoto, kushoto kwake kuna nn?
Hali kadhalika hiyo nhi ya kulia, kulia kwake kuna nn?
 
Mada inahusu mkandamizo wa hewa, sio mvutano wa sumaku
 
Swali nzuri....

Kama unataka kujua kuhusu hilo, ni vyema ukaamua kufanya tafiti zaidi kuhusu dunia yenye umbo la CD

Ukihitaji kitabu nipo tayari kukupa
 
Mada inahusu mkandamizo wa hewa, sio mvutano wa sumaku
Ndo nakwambia dunia inausumaku, huu usumaku unasukuma hizi solar storm hazifiki chini.
Solar storm inaweza kuondoka na atmosphere ikipiga kwenye uso wa sayari so usumaku wa dunia unatengeneza kama shield zinaishia juu juu huko
 
Kama ukingo ni uso wa dunia, ukingo mwingine wa upande wa juu ni upi?
Siyo lazima ukingo wa juu uwepo, kama unavyoona kwenye gesi iliyomo ndani ya mtungi wake.

Lakini kama dhana ya ukingo wa chini na juu ni wa lazima kwako ili uafiki, naweza kusema kwamba ukingo wa juu ni ileile kani mvutano wa dunia.

Molekyuli iliyoko juu zaidi kwenye ukingo wa hewa hiyo, bado huvutwa na kani ya dunia, licha ya kwamba kani hiyo ni ndogo ikilinganishwa na ile inayoshinikiza molekyuli iliyo karibu zaidi na uso wa dunia.

Ichukulie kani mvutano wa dunia kama neti fulani hivi kubwa mno iliyotandwa kuuzunguka ukanda wote wa dunia huko angani, inayoshikilia kila kitu, ukiwemo pia uowevu, vibaki kwenye uso wa dunia.
 
Ndo nakwambia dunia inausumaku, huu usumaku unasukuma hizi solar storm hazifiki chini.
Solar storm inaweza kuondoka na atmosphere ikipiga kwenye uso wa sayari so usumaku wa dunia unatengeneza kama shield zinaishia juu juu huko
Huo usumsku unahusiana kivipi na mkandamizo wa hewa?
 
Huo usumsku unahusiana kivipi na mkandamizo wa hewa?
Jaalia hapa unachembe za vumbi ukizipuliza zinafanyaje??? The same solar storm hupelekea kuondosha hewa kwenye sayari. Usumaku wa dunia unasukuma hizi solar storm hazifiki on the lower atmosphere
Sayari kama mirihi haina atmosphere kubwa kama dunia kwasababu tabaka hewa laje linaondoshwa na hizi solar storm coz haina nguvu kubwa ya usumaku ya kuzuia isifike kwenye atmosphere ya chini
 
Huo usumsku unahusiana kivipi na mkandamizo wa hewa?
Usumaku wa dunia ni kama neti kubwa sana iliyofungwa kuzunguka hizo molekyuli.

Kwa sababu zinavutwa kuja kwenye uso wa dunia, basi zinasababisha mgandamizo au shinikizo la hewa.

Ni sawa na Pawa Mabula awafunge kamba pamoja umati wa watu na kuwasokomeza kwake.

Usiniambie kwamba hawatobanana; hawatoumia kwa msongamano wao.

Kwa nini waumie? Shinikizo, mgandamizo, baby!!!
 
Siyo lazima ukingo wa juu uwepo, kama unavyoona kwenye gesi iliyomo ndani ya mtungi wake.

Lakini kama dhana ya ukingo wa chini na juu ni wa lazima kwako ili uafiki, naweza kusema kwamba ukingo wa juu ni ileile kani mvutano wa dunia.
Hiyo kani au mvutano haiathiriki na mzunguko mkali wa dunia?
 
Ni vipimo gani hutumika kupima kasi au nguvu ya huo mvutano kati ya atmosphere na uso wa dunia?
 
Kama ukingo ni uso wa dunia, ukingo mwingine wa upande wa juu ni upi?
Hivi unajua gesi zinatofautiana??

Unajua kitu kikiwa compressed kinakuwaje??

Unajua maji yenye shinikizo kubwa (bar 6000) yanaweza kukata chuma?
 
Swali nzuri....

Kama unataka kujua kuhusu hilo, ni vyema ukaamua kufanya tafiti zaidi kuhusu dunia yenye umbo la CD

Ukihitaji kitabu nipo tayari kukupa
Jibu bas si ni chap tu hilo jibu kwani linahitaji nn kujib?
Kitabu utaniambia ntaenda kusoma kwa nyongeza
 
Jibu bas si ni chap tu hilo jibu kwani linahitaji nn kujib?
Kitabu utaniambia ntaenda kusoma kwa nyongeza
Hiyo CD imezungukwa na barafu ambayo ni kama ukingo wa bahari, kama ilivyo kwa ukingo wa maji ya mtoni(river bank)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…