Wenye nguvu wanajitahidi kila mahali kuhakikisha hakuna maelewano duniani ili iwe rahisi kwa kutawala. Walianza katika ngazi ya taifa kwa taifa, sasa wamegeukia katika familia kwa kupitia kitu kinachoitwa Jinsia na Haki za Binadamu. Sasa hivi hata watoto hawaguswi, mashuleni walimu wameisha tupilia mbali viboko. Mnawaonaje wanafunzi kwenye hizo dala dala? Kabla ya ujio wa wakoloni Babu zetu hawakufahamu hilo neno la Jinsia lakini familia zilikuwa na maadili na zilidumu, tofauiti na sasa ambapo kuna ndo za miezi mitatu. Kazi ya Utandawazi hiyo, mtu utambakaje mke wako. Hapo lazima kulikuwa na kutokuelewana.