Kama hujarasimisha biashara yako jiandae kukutana na rungu la Serikali

kilagalila

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2018
Posts
320
Reaction score
154
Na.amiri kilagalila
mc.amiri,mr.mtaani
Kwa mjasiliamali na mfanyabiashara yeyote Tanzania ukitaka uendelee kufanya shughuli zako kwa uhuru zaidi basi ujue tu lazima ufuate utaratibu.

Ni kwambie tu kwa sasa hata machinga yaani Yule mfanyabiashara wa chini kabisa mpango ni kuwa ndani ya kitengo maalumu cha serikali tena kinachosimamiwa na ofisi ya Rais Ikulu.

Ngoja nikumegee jambo, leo hii nimefanikiwa kuhudhuria semina ya wajasiliamali mkoani Njombe katika ukumbi wa Turbo uliopo mjini Njombe, na kujifunza mambo tofauti tofauti kutoka kwa taasisi za kibenk, NSSSF,TRA na taasisi nyingine mbali mbali.

Lakini moja ya mada kubwa iliyotolewa kwa wajasiriamali ni hii ya urasimishaji wa biashara iliyotolewa na afisa wa biasahara MR.KAYOMBO kutoka ofisi ya halmashauri ya mji wa Njombe.

Jambo lililonivutia kuandika uzi huu ni pamoja na maada hiyo ambapo nimeona kabisa kwa sasa kuna mambo mengi ambayo mjasiriamali unatakiwa kuyafanya ili uweze kuaminika na kukubaliwa kibiashara zaidi unapohitaji kupata mikopo katika taasisi hizi za kifedha, miongoni mwa hayo mambo ni pamoja na kuwa na leseni ya biashara inayotolewa na halmashauri ya mji au zile zinazotolewa na halmashauri kuu na leseni hizi ili upate kuna sifa zake ambapo kwanza ni lazima uwe Mtanzania,uwe na akili timamu,uwe hujawahi kushtakiwa na makosa ya jinai lakini pia uwe na umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea.

Lakini pia kuna jambo jingine la kuwa na leseni ya makazi (nyumba) kutolewa kwenye miji na halmashauri husika kwa kuwa nayo kuelekea kwenye urasimishaji wa biashara itaweza kusaidia katika upatikanaji wa mikopo.

Katika utangulizi wa semina ya leo limetolewa ufafanuzi neno MKURABITA ambalo awali lilikuwa likiwachanganya watu wengi huku likiwa na maana ya “mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania”. Na ni mpango ulioanzishwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.mpango huu unasimamiwa na ofisi ya Rais Ikulu.

Lakini pia nini maana ya urasimishaji wa biashara? Maana yake ni kujenga uwezo kwa mfanyabiashara ili aweze kufanya biashara kwenye mfumo rasmi,
-kuondoa vikwazo vya sheria na kanuni ili kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwenye mfumo rasmi.
Biashara iliyorasmi ina sifa gani?
.Imesajiliwa
-jina la biashara
-kampuni
-ubia
.Ina mahali maalumu pa kufanyia biashara
.Biashara yenyewe iwe ina akaunti benki
.Inatunza kumbu kumbu za mahesabu
.Inatofautisha mali binafsi na mali za biashara
.Imesajiliwa kama mlipa kodi
.Ina wafanyakazi wenye mikataba ya kudumu
.Ina mahusiano na mifuko ya jamii
.Ina zingatia sheria za kazi

Je kuna faida gani kwa kufanya biashara kwenye mfumo rasmi
Mosi ni rahisi kupanua mtaji,pili biashara itaendeshwa kisheria na katika eneo maalumu,tatu hakuna bugudha katika toka mamlaka za serikali,wafanyakazi wanamikataba ya ajira hivyo wanakuwa na usalama kazini,kumbu kumbu za mahesabu zinatunzwa vizuri na hivyo kuweza kujua faida na hasara ya biashara,Ni rahisi kupata mikopo toka benki na taasisis nyingine za fedha,biasahar itaweza kukua sambamba na ukuaji wa soko la ndani,ni rais kufanya biashara na watu wengi zaidi,uhakika wa kupata faida ni mkubwa zaidi,ni rahisi kuingia ubia na watu/mashirika toka nje ya nchi.

Ni hayo tu mjasiriamali mwenzangu usipofanya hivyo jiandae kufanya biashara kwa kukimbizana na hawa migambo wasumbufu wa miji tena wale wenye lungu za sifa kwa kuwa mafunzo yao hufungwa na wakuu wa wilaya na mikoa.

MWISHO======================================================
 
Ni hayo tu mjasiriamali mwenzangu usipofanya hivyo jiandae kufanya biashara kwa kukimbizana na hawa migambo wasumbufu wa miji tena wale wenye lungu za sifa kwa kuwa mafunzo yao hufungwa na wakuu wa wilaya na mikoa.
Na iki kepengele kimefundishwa kwenye hiyo semina?
 
Hivi una biashara yenye mtaji wa laki nne, hizi gharama zilizotajwa ikiwa ni pamoja na kutoa ajira ya kudumu kwa wafanyakazi kadhaa, pia kulipa kodi ya serikali utabakiwa na nini ununue bidhaa za kuuzwa hapo dukani? Hayo ndo mazingira magumu kwa wafanyabiashara wadogo.
 
Ni bora kama unajua biashara yako ni ndogo ifanye mwenyewe na familia yako vizuri kwa ufasaha na uendane na serikali yako taratibu kuliko ukajitia wazimu wa kuweka msaidizi halafu ukahudhuria semina hizi utahisi kwanza unaonewa mwenyewe kumbe ni wajibu wetu kulipa hizo kodi stahiki lakini pili utadondosha chozi kama ni mwepesi kuona kwamba unamuonea kijana wako anayetafuta ridhiki.
 
Kwa mazingira haya ni ngumu sana mtu wa chini kutoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…